Rc njombe, christopher ole sendeka akamata gari la kubeba maji likiwa limebeba wafanyakazi 30

Na Amiri Kilagalila-Njombe

Mkuu
wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ametoa onyo kali kwa
makampuni ya ujenzi mkoani humo kutumia magari ya mizigo kinyume na
taratibu, kutokana na kuona gari maalumu la kubebea maji likiwa
limepakia wafanyakazi wanaofikia 30 wa kampuni ya CHICCO inayojenga
barabara kwa kiwango cha lami kutoka Njombe –Moronga kwenda Makete
wakiwa wamepakiwa juu ya roli  la kubebea maji (Boza).



Akiwa
kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye
urefu wa km 53.9, Mheshimiwa Ole Sendeka ameyataka makampuni
yanayotekeleza mradi wa kitaifa wa ujenzi wa barabara za lami na kiwango
cha zege ndani ya mkoa wa Njombe kuhakikisha wanatumia gari maalum la
kubeba wafanyakazi wao na si kuwapakia kwenye magari yasiyoruhusiwa
kubeba abiria ili kuepusha ajari, huku madereva wakitakiwa kutii sheria
za usalama barabarani..

“Ni
kwanini mkae juu ya boza,kwa hiyo kila siku mnabebana hivi? Kuanzia leo
biashara ya kuwapakia hawa wanaokwenda kutengeneza mitaro juu ya boza
ife,muiteni huyo meneja wenu mchina na msaidizi wake na HR wenu mripoti
ofisini kwangu’anasema Ole Sendeka

Hata
hivyo dereva wa gari la kampuni ya CHICCO ambaye alinaswa akiwa amevunja
sheria za usalama barabarani kwa kupakia wafanyakazi juu ya roli la
kubeba maji kinyume na sheria alipohojiwa sababu za kufanya hivyo
alisema kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria lakini wamekuwa wakifanya
kutokana na mazingira yao ya kazi yalivyo

Kufuatia
hali hiyo, kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa
alimwagiza mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Njombe (RTO)
kuchukua hatua mara moja.

“Mtakufa ninyi hiki mnachofanya ni hatari na nimeshapiga simu kwa RTO”anasema Hamis issa