Rc shigella: nchi haiwezi kujitegemea kama watanzania hawatalipa kodi

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao cha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa Jiji la Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa kikao hicho

 Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao hicho

 MKUU
wa Mkoa wa Tanga katikati akisisitiza jambo akiwa na Meneja wa TRA Mkoa
wa Tanga Specioza Owure kulia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga
Mhandisi Zena Said kushoto wakati wa kikao hicho

 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia akiwa kwenye kikao hicho

 Afisa
Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto akiwa na
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia wakifuatilia masuala
mbalimbali kwenye kikao hicho

 MENEJA wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese (Aliyevaa suti ya darkblue) kulia akiwa na wadau wengine wakifuatilia kikao hicho

 KAMANDA
wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa wakifuatilia kikao hicho

MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Mkwakwani Jijini Tanga akifuatilia kikao hicho 

 Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho wakiwemo wafanyabiashara  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu 

Elirehema
Kimambo ni Meneja Msaidizi Ukaguzi wa Kodi TRA Mkoa wa Tanga akati wa
kikao hicho na kushoto ni Meneja Msaidizi Madeni ya Kodi TRA Mkoa wa
tanga Lucas Kaigarula

 Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho wakiwemo wafanyabiashara  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo amekutana na
wafanyabiashara wa Jiji la Tanga kusikiliza kero zao huku akiwaambia kwamba nchi
haiwezi kujitegemea iwapo watanzania hawatalipa kodi ambayo wanapaswa kufanya
hivyo.
RC Shigella aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha
kusikiliza kero za wafanyaabiashara wa Jiji la Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku akieleza pia kwamba serikali haiwezi kujitegemea
iwapo watu hawataridhia kulipa kodi bila kushurutisha.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Tanga Mhandisi Zena Saidi,Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Katibu
Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi
Mayeji,wafanyabiashara na viongozi mbalimbali.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba pia serikali haiwezi
kujitegemea iwapo watu hawataridhia kulipa kodi bila kushurutishwa huku
akisisitiza kwamba kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt Magufuli ni kuhakikisha
anasimamia mapato yanakusanywa.
Alisema kwamba serikali ina matarajio makubwa kwamba
nchi katika misingi imara iliyoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ya dhana ya kujitegemea kwamba watanzania wanajitegemea
wenyewe kwenye mipango yao, kuitekeleza na kuifanisi.
Aidha alisema watanzania wanajitegemea kwenye kutekeleza
mipango yao na kufanikisha na moja ya chanzo cha cha mapato ni kuhakikisha kodi
inalipwa na ndio maana serikali ya Rais Dkt John Magufuli imeweka jitihada zake
kubwa katika kuhakikisha watanzania tunajitegemea.
“Lakini pia hatuna mjomba mwengine ambaye tunaweza
kumuomba msaada na Serikali ya awamu ya tano sio ya kupiga magoti na rais wetu
tunamfahamu matumaini yake macho yake yapo kwa watanzania kuhakikisha wana
simamia miradi”Alisema.
Alisema miradi yote mkubwa inayoendelea inahitaji fedha
ili iweze kujiendesha na hilo linatokana na watanzania kulipa kodi hivyo
watambue kwamba kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Anasema kuioa ulipa kodi ndio wanaona ujenzi wa
barabara ya poangani Tanga mkandarasi amekabidhiwa eneo na wiki ijayo ili
barabara hiyo iweze kutengenezwa, bandari ya Tanga ilikuwa na tatizo la muda
mrefu tayari ufumbuzi wake umanza kupatikana kuna mashine majini inachimba kina
kutoka cha sasa mpaka kufikia mita 14 hadi 15 ili kuruhusu meli zinazokwenda
Dar ziwezi kufika Tanga.
Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Meneja wa TRA
Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kikao hicho kinakatokana na agizo la Naibu
Kamisha wa TRA Msafiri Mbibo ambaye aliagiza kuandaa kikoa kingine ambacho
kitajumuisha mamlaka hiyo na taasisi nyengine zinazohusika na wafanyabiashara.

Alisema kikao hicho ni kutiia agizo la Naibu Kamishna
huyo ambapo Mkuu huyo wa mkoa alihaidi kwamba atakuwa mgeni rasmi kusimamia na
kusikiliza kero za wafanyabiashara hao.