Rc shinyanga aipongeza ewura kwa uwazi upangaji bei za maji shuwasa

 Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji ( EWURA) kwa kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali kutoa
maoni yao kuhusu ombi la marekebisho ya bei za majisafi na usafi wa mazingira
za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), 22
Agosti 2023.

 

Pongezi hizo
zilitolewa kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude,
aliyemuwakilisha RC huyo na kueleza kuwa, EWURA inastahili kupongezwa kwa kuendelea
kusimamia na kutekeleza sera ya uwazi kwa vitendo.

 

kwa niba ya RC Shinyanga nawasilisha pongezi kwenu EWURA kwa kuendelea
kuwashirikisha wananchi kutoa uamuzi wa mustakabali wa maisha yao ya kila
siku”.
Alisema Mkude

 

Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. George Mhina alisema, uwazi ni moja ya nguzo ya
maadili ya EWURA hivyo Mamlaka itaendelea kuzingatia suala hilo katika
utekelezaji wa majukumu yake.

 

Mkurugezi Mtedaji wa
SHUWASA Mha.Yusuph Katopola, ameeleza kuwa, ombi la kurekebisha bei za maji na
usafi wa mazingira ni kwa kipindi cha miaka mitatu yaani 2023/4; 2024/25 na
2025/26; likianisha kuongezeka kwa gharama za huduma kwa wastani wa asilimia
47.

 

Mkurugenzi wa mamlaka ya
majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhendisi Yusuph Katopola akiwasilisha
mapendekezo ya bei za maji kwa wadau  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM
Mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa EWURA kanda ya ziwa  George Mhina akizungumza kwenye taftishi
iliyolenga kupokea ombi la kurekebisha bei za maji kutoka mamlaka ya maji safi
na usafi wa mazingira Shinyanga Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa
mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mhe. Joseph Mkunde awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, uliolenga kupokea mapendekezo ya
bei mpya za maji  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa
Shinyanga.

Mwakilishi kutoka Baraza
la ushauri la serikali (GCC) Mr. Julius Mwambaso akitoa ushauri kwenye mkutano
huo  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi kutoka Baraza
la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na Maji EWURA CCC Bwana Joseph
Ndatala akitoa ushauri kwenye mkutano huo  Jumanne Agosti 22,2023 katika
ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

 

Mkutano ukiendelea  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga