Rsa waiomba serikali kuifanyia mabadiliko sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma kutoka Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ( RSA) Ally Nurdin  
Na.Vero Ignatus,Pwani.
Taasisi ya Mabalozi wa usalama barabarani (RSA)kwa
kushirikiana  na wadau wengine wameiomba serikali kuangalia upya sheria
ya usalama barabarani nchini Tanzania iliyotungwa mwaka 1973 ambapo
sheria hiyo imerithi kanuni mbalimbali zilizotungwa tangia mwaka 1933
ambapo zimeendelea kuboreswa kipindi hadi kipindi.
Akizungumza Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma( RSA) Ally Nurdin  amesema
kuwa hadi kufikia mwaka 2018 marekebisho makubwa ya sheria hiyo ya
usalama barabarani sura ya 168 ni yale ambayo yalifanyika mwaka 1996.
”Marekebisho
hayo yalifuata baada ya hapo yalihusu ongezeko la faini tu bila kugusa
vipengele vya msingi vya sheria yenyewe kwasababu tangu wakati huo hadi
sasa idadi ya magari inaongezeka barabarani idadi ya watumiaji wa vyombo
vya moto inaongezeka pamoja na vyombo tofautitofauti ambavyo havikuwepo
wakati huo pia vinatumika barabarani na tabia za watumiaji wa vyombo
hivyo zinabadilika kwa kuongezeka tabia nyingi mpya ambazo
hazikuwepo”Alisema
Nurdin alimesema
kuwa vipengele vinavyotakiwa kufanyiwa marekebisho ni pamoja na kifungu
cha 5 kuhusu usajili wa magari lakini hakiweki wazi iwapo usajili huo
ni ule wa kieletroniki ili mmiliki wa gari asilazimike kutembea na gari
muda wote,kwasababu kadi inaweza kuwepo mkwenye simu au kwenye App
fulani,ambapo sheria ni wakati wake kutambua jambo hilo.
Amesema
kuhusu umri wa kumiliki gari kifungu cha 10(20)sheria ilivyo sasa
inamapungufu inampiga marufuku mtu aliye chini ya miaka 18 kumiliki gari
hata hivyo aliye na miaka 14 anaruhusiwa kumiliki pikipiki,amesema yapo
maoni kwamba sheria hiyo isiruhusu kabisa aliye chini ya miaka 18
asimiliki pikipiki wala gari japo kuwa maoni mengine yanakinzana na
kusema aruhusiwe.
”Swali
linakuja je mmiliki akitaka kuuza atauzaje wakati kuna mikataba
inayosema kuwa aliyechini ya miaka 18 haruhusiwi kui ngia katika
mkataba,wakati huo huo ikitokea kwamba kuna makosa yanamhusu mmiliki wa
gari kushtakiwa au kufungwa au kulipa faini je atalipaje kwa mmiliki wa
umri wa chini ya miaka 18?” Aliuliza 
Aidha
amesema kuwa katika faini kutumia gari bila kusajili sheria hiyo katika
kifungu cha 8(2) ambapo faini yake ni shilingi elfu hamsini tu au
kifungo kisichopungua miaka mitano,amesema faini hiyo italipwa
mahakamani iwapo mtuhumiwa atakutwa na hatia,jambo ambalo barabrani
faini yake ni shilingi elfu thelathini.
Amesema kuwa kifungu cha 11(4)kuharibu
au kubadili alama za utambulisho wa gari inamtaka alipe faini ya
shilingi elfu kumi ambapo adhabu hiyo ni ndogo kwa wanaofanya makusudi
ili wasitambulike wanapofanya makosa,amesema kifungu cha 14(5) kosa
la kutoweka au kuficha alama ama kuongeza alama za utambulisho wa gari
adhabu yake ni shilingi elfu tano ambapo haimfanyi mhusika kuijutia
kosa.
Aidha Amesema kifungu cha 18 kinahusu
kosa la kutumia gari bila alama za utambulisho au kutumia alama za
utambulisho wa gari lingine au kutoa taarifa za uongo kuhusu usajili wa
gari ambapo kosa hilo kwa sasa adhabu yake shilingi 10,000 Kwani makosa ya makusudi kama haya adhabu yake ni ndogo,k
ifungu cha 19 kosa la kuendesha gari pasipokuwa na leseni halali au kumruhusu asiye na leseni adhabu ya kosa hilo nayo ni shilingi 10,000
Ameainisha kuwa kifungu cha 21(1) leseni
ya lena kwa dereva mwanafunzi wa udereva wa pikipiki amesema sheria
iliyop[o sasa haimlazimishi anayejifunza kukata leseni ya lena kabla ya
kuanza kujifunza kuendesha hivyo ni vyema seria ikaweka hitaji hilo kwa
madereva wa pikipiki na bajaji,kifungu cha 23(7)kinachompa mamlaka
mtahini wa udereva kumpitisha dereva kwa amefaulu na hivyo anafaa kupewa
leseni na msajili.
”Kifungu
hiki hakimwajibishi afisa yeyote wa serikali au mtahini au mtu yeyote
aliyejiusisha katika kufanya udanganyifu wa kumtafutia mtu leseni ya
usereva ambaye hana sifa za zinazostahili,hivyo sheria na kanuni
haziweki bayana sifa ambazo anatakiwa mtahini kuwa nazo huyo anayetakiwa
kutahini madereva wanafunzi ,hivyo ifike wakati sasa sheria ikafanyiwa
marekebisho ili kuweza kuwaadhibu Maofisa kama hawa”alisema.
Kwa
upande ambao unamruhusu sajili kumpa mtu leseni ya udereva kwa kutumia
uzoefu wake bila kupitia shule kifungu hiki kwasasa yafaa kirekebishwe
kwa kumtaka kila mtu kupita katika shule ya udereva uliyo sajiliwa rasmi
kwa ajili ya kufundisha madereva kabla ya kupata leseni.
kwa upande wake mkurugezi msaidizi wa habari na mawasiliano kwa umma kutoka taasisi ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA )Ramadhani Msangi aliainisha
baadhi ya orodha ya makosa yanayoweza kumfanya mtu afungiwe leseni yake
au kufutiwa na (mahakama lazima ifungie au kufuta leseni)kifungu cha
27(1)kinatoa orodaha ya makosa amabayo kwayo leseni inaweza kufungiwa au
kufutwa kwa lazima ya mahakama
Amesema kuwa makosa lazima ambayo yanaweza kufutwa leseni kwa muda wa miaka mitatu kwa
mujibu wa kifungu cha cha sheria 27(1) dereva anaweza kufutiwa leseni
na mahakama,iwapo kwa mara ya kwanza ametenda makosa  kama vile
kusababisa madhara ya mwili au kifo kwa njia ya uendeshaji wa
hatari,kutokuwa makini barabarani,kuendesha kwa papara au kwa
hatari,kuendesha gari dereva huku akiwa amekunywa pombe au ametumia
madawa ya kulevya,kuendesha akiwa hana leseni halali au wakati leseni
ikiwa imefutwa au kufungiwa
”Dereva
anaweza kufungiwa au kufutiwa leseni iwapo atakuwa ametenda makosa ya
hatari kwa mara ya kwanza kutokuwa makini barabarani,matumizi mabaya ya
gari lake barabarani bila kujali watumiaji wengine wa barabara ,kutokuifanya hai leseni yake na kuondolewa sifa za kuendesha gari”Alisema
Aidha ameyataja makosa mengine kuwa ni sambamba na dereva kufungiwa leseni kwa muda wa miezi sita iwapo
kwa mara ya pili ametenda makosa yaleyele ya awali,kufungiwa kuendesha
gari kwa muda wamiezi 12 iwapo atakuwa hajatimiza wajibu wake baada ya
ajali mfano kusaidia majeruhi wakati ilikuwa salama kufanya hivyo au
kutoripoti ajali kwa wakati,
Pia dereva anaweza kufungiwa leseni kutokana na ulevi iwapo
atakuwa na kiwanmgo cha ulevi kisichozidi 150mg katika 100mls za damu
atafungiwa kuendesha kwa miezi sita na endapo atarudia atafungiwa kwa
miaka mitatu,kilevi kilichozidi 150mg atafungiwa kuendesha kwa miaka
miwili na endapo atarudia atafungiwa kwa miaka sita.
Amesema mapendekezo katika sehemu hii ni kuondoa kosa la kifungu cha 40:kusababisha madhara kwa mwili au kifo kupitia uendeshaji wa hatari linalojitokeza katika kifungu kidofo cha kwanza cha aya ya a-d ya kifungu cha 27(1)madereva hatari wapewe adhabu kali zaidi wakati wale madereva wazembe wapewe adhabu ya chini kidogo
Aidha inapendekezwa kipengele kuhusu makosa ya ulevi katika kifungu cha 27(1)kifutwe chote ili adhabu zake zibakie katika kifungu cha 44-49 ambapo
kinahusu nmakosa yanayohusiana na ulevi,pia wameshuri katika sehemu
hiyo yachambuliwe vizuri ili wanaoendesha kwa hatari barabarani bila
kujali watu wengine leseni zao zifunguiwe kwa muda mrefu zaidi na katika
kipindi ambapo leseni zao  zifungiwe walazimishwe kurudi shule.
Amehitimisha
kwa kusema kuwa wanahitaji marekebisho ya sheria ya usalama barabarani
kwa kuyapa kipaumbele yanatakiwa ya haraka ni yale ya yanayohusu
ulevi,mwendokasi,ufungaji wa mikanda,uvaaji wa kofia ngumu (helmeti)
magari madogo,amesema hayo ndiyo mambo ambayo RSA wa kuchagiza
marekebisho ya sheria ya usalama barabarani  imeyalenga kwa sasa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *