Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza
wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa
kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya
Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mratibu wa Mradi wa AgResults
Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema akizungumza wakati
wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa
kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya
Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mshirika wa Price Water house
Cooper (PwC), Bw.Nelson Msuya wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza
wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani
kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Steve Michael wakati wa hafla ya
kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika
kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa,
Pwani, Morogoro na Tanga.
Wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo
nchiniwakifuatilia hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita
waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji
walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Wauza pembejeo waliochaguliwa
kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya
Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga wakipatiwa vyeti mara baada ya
kufanya vizuri katika sekta hiyo.Zoezi la utoaji vyeti limefanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Sekta ya mifugo sasa inachangia
uchumi wa nchi zaidi ya asilimia 7.4% na mwaka huu wa fedha unaoisha,
sekta hii inakuwa kwa asilimia 5% lengo likiwa kufikia mara mbili kwenye
mchango wa uchumi na kuweza kufikia angalau asilimia 15 ifikapo mwaka
2025.
Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole
Gabriel wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji wa pembejeo sita
waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji
walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Amesema uzalishaji wa maziwa nchini
umefikia bilioni 3.4 ikiwa maziwa yanayosindikwa ni lita milioni 75 hii
inamaana inaleta wawekezaji wengi kuja kuchakata na kuleta thamani
kwasababu wateja wananunua maziwa ambayo yameongezwa thamani .
“Takwimu zinaonesha katika lita
bilioni 3.4 maziwa yanayotka kwenye ng’ombe wa kienyeji ni lita bilioni
2.38 kwahiyo lita bilioni 1.2 tu zinaonesha zinatokana na ng’ombe wa
maziwa”. Amesema Prof. Ole Gabriel.
Aidha amesema Tanzania ni nchi ya
pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ambapo inazaidi ya ng’ombe
milioni 33.9 na mbuzi wameshafika zaidi ya milioni 22 wakati kondoo
wamefika takribani milioni 6, kuku wamefikia milioni 87.7.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa
AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema amesema
kuwa kupitia mradi huo wana matokeo mazuri wameyaona ambapo kuna
ng’ombe 558 tayari wana mimba na wengine tayari wameshapata watoto pia
kuna ng’ombe 336 ambao wameogeshwa kitaalamu na vilevile kuna ng’ombe 62
ambao hao wamepata chanjo kuanzia mbili na kuendelea.
“Wauza pembejeo hawa wameweza
kuwafikia wafugaji 2776 na kuuza pembejeo nne ambazo ni vidhibiti
vimelea, Chanjo, lishe uhimilishaji pia mpaka sasa tuna ng’ombe 17,000
ambao wamepata huduma mbalimbali za lishe katika kuongeza afya bora na
pia kuweza kupata maziwa yaliyobora”. Amesema Bi.Mrema.
Amesema kuwa mradi huo una malengo
matatu ambapo lengo la kwanza ni kuongeza uzalishaji na tija ya maziwa
kwa wafugaji wadogowadogo, kuongeza kipato kwa wafugaji wadogowadogo wa
maziwa, kuleta uwiano sahihi na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa
shughuli katika sekta ya maziwa .
Hata hivyo Bi.Mrema amesema washiriki
sita wa mradi huo kutoka sekta binafsi wamepata tuzo na motisha ya dola
za kimarekani 27,000 kwa pembejeo 4116 zilizokamilika ili waweze
kuendelea kutoa huduma na kuongeza uzalishaji wa maziwa na kukidhi soko
la Tanzania.