Serikali kuendelea kukomesha vitendo vya ukatili jiji la arusha

Sehemu ya washiriki wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wanawake Jiji la Arusha yalioadhimishwa kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid Jijini Hapa leo.picha zote na Mahmoud Ahmad Arusha.
Meza kuu akiwamo mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Poul Mattsern Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni Meya Mstaafu Kalist Lazaro Mwenyekiti wa UWT mkoa Jasmini Bachu Mwenyekiti wa UWT Jiji la Arusha wakifuatilia maadhimisho hayo jijini Arusha.

Wakinamama wakishangilia na kucheza kwenye maadhimisho ya siku yao leo jijini Arusha picha Mahmoud Ahmad Arusha.
Sehemu ya bango la Taasisi ya maendeleo Tengeru wakiwa kwenye maandamano ya siku ya wanawake mkoa wa Arusha iliyofanyika kwenye viwanja vya Sheikh Amri Kaluta Abeid Jijini Hapa leo 

Maandamano yakiingia uwanjani

Wanafunzi wa kike wakiwa kwenye maadhimisho hayo kupinga Ndoa za utotoni zinazokatisha ndoto zao za kumaliza masomo.

Wakinamama wakiandamana wakiingia kwenye viwanja vya Sheikh Amri Kaluta Abeid kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo jijini Arusha

Maandamano yakiendelea 

Wakinamama wakipata nafasi ya kucheza katika kusherehekea siku yao ya wanawake duniani 

Mgeni Rasmi akipokea maandamano ya kinamama wa Jiji la Arusha kwenye maadhimisho ya siku ya kinamama duniani leo jijini Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na viongozi mbalimbali wakisoma mabango kwenye siku ya wanawake Jiji la Arusha Leo picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake

Merry kisaka Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Arusha  akiongea kwenye maadhimisho hayo jijini Arusha leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

SERIKALI wilaya ya Arusha,imesema kuwa imejipanga ili kuondoa na kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana ambavyo huzima ndoto na matarajio yao katika maisha .
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro, ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua kongamano la maadhimisho ya siku ya wanawake Ulimwenguni iliyofanyika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeidi,Jijijini Arusha.
Mkuu wa wilaya, amesema kuwa bado kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana na kueleza kuwa Serikali itaunganisha nguvu zake na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kukomesha ukatili wa kijinsia na kuchukua hatu pindi inapolazimika
Amesema chimbuko la  kudai haki na usawa wea kijinsia lilianzishwa na wanawake nchini Marekani mwaka 1919 walipodai haki zao kutokana na kulipwa ujira mdogo, kunyanyaswa  kiuchumi ,kisiasa na kijamii .
Amesema usawa wa kijinsia kwenye Jamii zetu unaathiriwa na maswala mbalimbali ya kijamii hasa wasichana ambao wapo shuleni ndio wahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kuzima ndoto na matarajio yao katika masomo na matokeo yake wanapata mimba.
Amesema kuwa serikali itaendelea kuwalinda wanawake na wasichana kwa kuimarisha Dawati la Jinsia katika Jeshi la Polisi,ambapo litawachukulia hatua stahiki wale wote watakaowakaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Pia amesema kuwa katika mwendelezo huo wa kumlinda wanafunzi wa kike, Afisa elimu, Waratibu elimu kata pamoja na watendaji wa kata wanaenda kutembelea shule mbalimbali na kutoa elimu ya kuwalinda wasichana dhidi ya vitendo vya ukatili .
Aidha ameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji kuwakamata watoto wanauuza mifuko kwenye masoko ambao wameacha shule na kuwarejesha shuleni ili waendelee na masomo yao.
Awali Grace Murro,kutoka shirika la World vision , akiwasilisha taarifa ya utafiti wa ukatli wa kijinsia kwa wanafunzi kwenye shule za sekondari, amesema kuwa kuna manyanyaso ambapo walimu wa masomo ya Biolojia huwa wanatumia lugha za uzalilishaji kwa wasichana.
Amesema baadhi ya walimu wa kike huwa wanatumia lugha za kuwadharirisha wasichana na hivyo kuwaondoa kwenye hali ya masomo na kusababisha kukosa usikivu  na kusisitiza kuwa kiwango cha ukatili ni kikubwa  kwenye shule za sekondari hivyo kukwamisha ndoto za wasichana kuendelea na masomo.