Serikali kuendelea kushirikiana na taasisi za dini, baraza la eid el fitr lafanyika mjini shinyanga ukabila, udini wakemewa

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi
ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi
amesema serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa Dini katika kuendeleza amani
na umoja Nchini.

Ameyasema
hayo leo April 22,2023 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na
waumini wa Dini ya kiislam kwenye 
Baraza la Eid El Fitr ambalo limefanyika katika  ukumbi wa Mikutano
uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani.

Naibu Waziri
Mhe. Paschal Patrobas Katambi amesema serikali inatambua umchango unaofanywa na
taasisi za Dini ambapo amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kushirikiana na
taasisi hizo ili kuendeleza umoja na amani ya Taifa.

Amewasihi
waislam kuendelea kuyaishi yale mema ambayo wamekuwa wakiyafanya katika kipindi
cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa ramadhan ikiwemo upendo, majitoleo, kusaidia
watu wenye mahitaji pamoja na kuombea Nchi na viongozi wa serikali.

Serikali yenu inawatambua inawaheshimu na
inawasikiliza tutaendelea kushirikiana siku zote kwenye mambo ya kiimani na
mambo mengine ya muhimu yasiyoya kijamii”.

“Tumemaliza
siku zetu hizi 30 lakini tuendelee kuyaishi yale ambayo tumeyaishi katika
kipindi chote cha mfungo lakini pili tuendelee kuwa na upendo, kuwa na moyo wa
subira, kutoa sadaka, kuwaombea wengine na kuwasaidia watu wenye uhitaji”.
amesema Mhe. Katambi

Aidha Mhe.
Katambi amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kukemea mmomonyoko wa maadili kwa
vijana huku akiwataka wazazi na walezi kufuatilia tabia za watoto wao ili
kuwaepusha kuingia kwenye makundi yasiyofaa.

Naibu Waziri
Mhe. Katambi amewahakikishia kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea
kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kutatua changamoto za
wananchi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Katika
Baraza hilo mjumbe wa BAKWATA Wilaya ya Shinyanga Bwana Hussen Mohamed Kheri
amesema risala ambapo mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe.
Paschal Patrobas Katambi amepokea na kuahidi kutatua changamoto zilizopo
ikiwemo changamoto ya usafiri pamoja na vyombo vya matangazo ( Vipaza sauti)
ili kuendelea huduma za kiimani.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail
Habib Makusanya amesisitiza upendo kwa watu wote huku akihimiza baadhi ya
vyama vya kisiasa Mkoa wa Shinyanga kuacha utengano wa kubagua Dini wala Kabila
na kwamba wanapaswa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kidini pamoja na
shughuli za kijamii.

“Hapa
Shinyanga kuna baadhi ya vyama vina udini kweli kweli na hasa nyakati za
uchaguzi ukifika utaona wanachaguana kwa kuangalia udini na yule ambaye atakuwa
siyo Dini yake atapigwa chini hili nimelifuatilia na nimeligundua hili
linatuvunjia heshima yetu kwahiyo sisi udini hatuutaki katika Mkoa wa Shinyanga
lakini pia kuna ukabila upo nao siyo mzuri katika Mkoa wetu”.
amesema
Sheikh Makusanya

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya
waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi
akizungumza leo April 22,2023 kwenye 
Baraza la Eid El Fitr
katika  ukumbi wa Mikutano uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya
zamani.

 Sheikh wa Mkoa
wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akizungumza kwenye  
Baraza
la Eid El Fitr katika  ukumbi wa Mikutano uliopo CCM Mkoa wa
Shinyanga NSSF ya zamani.

Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Suleiman Kategile akizungumza
kwenye Baraza la Eid El Fitr katika ukumbi wa mikutano uliopo CCM Mkoa wa
Shinyanga NSSF ya zamani.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya
waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi
 awali akipokelewa na Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Suleiman Kategile.

Baraza la Eid El Fitr likiendelea katika ukumbi wa mikutano
uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani leo April 22,2023

Baraza la Eid El Fitr likiendelea katika ukumbi wa mikutano
uliopo CCM Mkoa wa Shinyanga NSSF ya zamani leo April 22,2023