Na. Edward Kondela
Serikali
imewataka wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali Mkoani Mbeya
kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya
kutoingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa ya Ruaha na Pori la
Akiba la Ruangwa, hali ambayo imekuwa ikisababisha migogoro kati ya
wafugaji na askari wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), wanaolinda hifadhi hizo
ambapo baadhi ya migogoro hiyo imesababisha vifo vya wafugaji, askari
na mifugo.

Akizungumza Jumanne hii (19.11.2019) wakati wa kuhitimisha ziara ya siku
mbili ya makatibu wakuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara
ya Sheria na Katiba, waliozuru baadhi ya maeneo yenye migogoro katika
wilaya hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.
Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kuacha tabia ya kuingiza mifugo
katika maeneo ya hifadhi kwa ajili ya malisho kwa kuwa ni kinyume na
taratibu za nchi.

“Serikali inawataka wafugaji wote kufanya shughuli zao kwa kufuata
sheria na kutoingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi za taifa kwa kuwa
ni kinyume cha sheria pia serikali itaendelea kuhakikisha wafugaji
wanafanya shughuli zao kwa amani bila kubughudhiwa ili mradi wanafuata
sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya kutoingiza mifugo katika mashamba
ya wakulima.” Amesema Prof. Gabriel

Akizungumza kwa niaba ya makatibu wakuu wa wizara hizo, Prof. Gabriel
amefafanua kuwa kutokana na Tangazo la Serikali (GN) Na. 28 la Tarehe 14
mwezi Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha kutoka Kilometa za Mraba 5,878 hadi kufikia Kilometa za Mraba
20,226 hali hiyo imesababisha eneo la malisho kupungua kutoka hekta
259,000 za awali hadi 154,000 katika Wilaya za Chunya na Mbarali ambapo
amewataka wafugaji katika wilaya hizo kuheshimu tangazo hilo wakati
serikali ikifanyia kazi maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuainishwa kwa vijiji
vilivyopo katika maeneo ya hifadhi ili maboresho yaweze kufanyika kwa
maslahi ya vijiji hivyo.

Katika ziara hiyo ya makatibu wakuu kutoka wizara nne Mkoani Mbeya
uongozi wa TANAPA umekubali kutengeneza barabara za kuainisha mipaka ya
maeneo ya hifadhi na vijiji mara baada ya kuainishwa kwa mipaka mipya
kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutambuliwa kwa maeneo ya
vijiji na hifadhi za taifa ambalo tayari linafanyiwa kazi.

Kufuatia matukio ya mauaji ya askari mmoja wa TANAPA na askari mgambo
mmoja mwaka 2018 waliouawa na wafugaji wakati wakiswaga ng’ombe
waliokamatwa katika Hifadhi ya Ruaha kuelekea Kambi ya Nyota ya TANAPA
iliyopo Wilaya ya Mbarali na tukio la hivi karibuni la Tarehe 11 Mwezi
Oktoba 2019 la kuvamiwa kwa kambi hiyo na baadhi ya wafugaji wakiwa na
silaha za jadi kwa nia ya kukomboa mifugo iliyokamatwa katika Hifadhi ya
Ruaha hali iliyosababisha kijana mmoja wa wafugaji (19) kupigwa risasi
na askari wa TANAPA na ng’ombe 14 kuuawa, Katibu Mkuu Prof. Gabriel
amewataka wafugaji kutumia njia zisizo halali kukomboa mifugo
iliyokamatwa.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika Kijiji cha Igunda, Kata ya
Igava Wilayani Mbarali, katibu mkuu huyo amefafanua kwa wafugaji hao
kuwa kutokana na sheria na haki za wanyama duniani ni makosa kuua mnyama
bila kuwa na sababu za msingi hali iliyosababisha serikali kuchukua
hatua kwa askari wa TANAPA waliohusika kupiga ng’ombe hao risasi na
hivyo kuwataka wafugaji hao kuwa watulivu kwa kuwa suala hilo
linashughulikiwa na vyombo vya dola.

Aidha ameeleza kuwa kuwa pindi mifugo inapokamatwa na askari wa TANAPA
inapobainika kuingia kwenye maeneo ya hifadhi, wamiliki wa mifugo hiyo
wanapaswa kufuata taratibu za kisheria za kulipa faini na kukabidhiwa
mifugo yao na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wafugaji kujiepusha kuingiza
mifugo maeneo wasiyoruhusiwa yakiwemo ya Hifadhi za Taifa.

“Sisi viongozi wa Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo
ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba tunasikitishwa sana na matukio haya
ya mauaji kijana mdogo amefariki dunia kwa sababu ambazo zingeweza
kuepukika kwa kutaka kumdhuru askari kwa kutumia silaha za jadi akiwa na
wenzake takriban 20 ili kukomboa ng’ombe waliokamatwa hifadhini,
tunawaomba mjiepushe na matukio ya namna hii fuateni sheria na taratibu
za nchi ili mfuge bila bughudha.” Amefafanua Prof. Gabriel

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole
Gabriel akiwaongoza viongozi wenzake katika ziara hiyo akiwemo Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara
ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wamefika pia katika Kijiji
cha Lualaje Kata ya Lualaje Wilayani Chunya na kuzungumza na baadhi ya
wafugaji kufuatia matukio ya wafugaji hao kuingiza ng’ombe katika
Hifadhi ya Ruaha.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima
amewataka wafugaji hao kufuata sheria na taratibu za nchi na kwamba
jeshi la polisi litazidi kutoa ushirikiano kwa wafugaji hao katika
matukio mbalimbali yakiwemo ya kuwabaini baadhi ya wafugaji ambao
wamekuwa wakiingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi pamoja na
kujihusisha na uhalifu.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju
amewataka wafugaji kuwa watulivu na walitambue Tangazo la Serikali Na.
20 la Tarehe 14 mwezi Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kupunguza eneo la malisho katika Wilaya za
Chunya na Mbarali hali iliyosabisha baadhi ya maeneo waliyokuwa
wakiyamiliki kubadilishwa matumizi na kuwa ya hifadhi, ambapo suala hilo
tayari linafanyiwa kazi kwa maelekezo ya Rais Magufuli na kuwataka
kutoingiza mifugo yao katika eneo la hifadhi hadi serikali
itakapotangaza maamuzi mengine.

Kuhusu kuainishwa kwa mipaka kati ya vijiji na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
pamoja na Pori la Akiba la Ruangwa, akizungumza kwa niaba ya katibu
mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori
kutoka katika wizara hiyo Dkt. Maurus Msuha amesema serikali kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii itahakikisha inatuma timu ya wataamu
katika maeneo hayo ili kuweka alama maeneo ambayo wananchi yanawatatiza
kufahamu mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi ili kuondoa migogoro kati
ya maeneo ya wakulima na wafugaji na mipaka ya Hifadhi ya Ruaha na Pori
la Akiba la Ruangwa.

Baadhi ya wananchi katika Wilaya za Chunya na Mbarali waliopata fursa ya
kuzungumza wakati wa ziara ya makatibu wakuu kutoka Wizara za Mifugo na
Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba
wamesema wamefurahishwa na ziara hiyo na kwamba watazingatia maelekezo
waliyopatiwa ili kuhakikisha wanafuga kwa kufuata sheria na kwamba
watashirikiana na serikali ili kuwabaini baadhi ya wafugaji wanaokiuka
sheria na kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la
Akiba la Ruangwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamefafanua kuwa wamefurahishwa kwa
viongozi hao wa juu kutoka wizarani kufika hadi katika maeneo yao na
kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji na malisho
pamoja na kupata taarifa za matukio ambayo yamejitokeza katika wilaya
hizo kutoka mamlaka mbalimbali za serikali wakiwemo viongozi wa
serikali, wafugaji pamoja jeshi la polisi.

Awali kabla ya makatibu wakuu hao kutembelea wafugaji katika Wilaya za
Chunya na Mbarali, wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mbeya na kuwa na
mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila pamoja Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, ambapo Mhe. Chalamila amewaambia
serikali ya mkoa huo itaendelea kufanya kazi kwa kusimamia sheria na
kuwaasa viongozi wenzake wanapofika mkoani hapo kupata taarifa sahihi ya
mkoa kabla ya kufika katika maeneo mbalimbali kuzungumza na wananchi.

Aidha Mhe. Chalamila amebainisha kuwa migogoro ya wafugaji katika Wilaya
za Chunya na Mbarali ambao wamekuwa wakiingiza mifugo kwenye maeneo ya
Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa katika Mkoa wa Mbeya
unatokana na wafugaji kuwa na mifugo mingi tofauti na maeneo ya malisho,
hali ambayo imekuwa ikiulazimu uongozi wa mkoa kutoa elimu kwa wafugaji
juu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji kuwa na ng’ombe
wachache wanaoweza kuwapatia matokeo mazuri.

Ameongeza kuwa uongozi wa Mkoa wa Mbeya utazidi kusimamia na kutoruhusu
mifugo kuingizwa katika maeneo ya hifadhi pamoja na maeneo yaliyotengwa
kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa na
mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Katika ziara hiyo ya makatibu wakuu wanne Mkoani Mbeya, ikiongozwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole
Gabriel akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba
Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha
akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf
Mkenda, ilikuwa na lengo la kupata taarifa sahihi ya hali ya wafugaji
katika Wilaya za Chunya na Mbarali pamoja na kupata hadidu za rejea
ambazo wataalam watatumia katika kufanya mapitio na maboresho ya Tangazo
la Serikali (GN) Na. 28 la Mwaka 2008 ili iwe shirikishi na kupata
suluhu ya migogoro ya wakulima na wafugaji.

MWISHO