Serikali yawataka waajiri wa makocha kutoka nje kutoa taarifa zao tra ili walipe kodi

Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali
imezitaka timu zote za mpira zinazoajiri makocha na wachezaji kutoka
nje ya nchi kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya
waajiriwa walionao wanaotakiwa kulipa kodi.


Hayo
yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Nyongeza la
Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Selemani Nkamia, aliyetaka kujua Serikali
inatambuaje Kocha au Mchezaji wa Nje aliyelipa na asiyelipa kodi kwa
kuwa malipo yao hufanywa kiholela kwa kuwa hakuna mfumo rasmi.

Dkt.
Kijaji alisema kuwa Kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira ndani
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato
kulingana na kipato chake.

“Kila
mgeni akifikisha miezi 6 anahesabika ni mkazi (local resident) na
anapaswa kulipa kodi, ni jukumu la mwajiri kutoa taarifa ya nani
analipwa nini ili kodi zote stahili ziweze kulipwa kwa mujibu wa
sheria”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema
kuwa ulipaji wa kodi ya ajira ni kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato
ya mwaka 2004 na ni jukumu la mwajiri kwenda kutoa taarifa kwenye
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao wanaotakiwa
kulipa kodi hiyo.

Dkt.
Kijaji alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Sh.
milioni 1,733.6 zilikusanywa kama malipo ya kodi ya ajira kutoka kwa
makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *