Sherehe za kicoba kugawana faida zageuka kilio arusha

 Image result for vicoba
 
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Sherehe za kugawana faida katika  kikundi cha ujasiriamali cha  Imani ambazo zilikuwa zifanyike mapema jana zimegeuka kilio kwa wanachama wa kikundi hicho zaidi ya 20 kwa kuangua vilio na kuzimia ukumbini baada ya taarifa ya upotevu wa fedha zaidi ya milioni 40 zinazodaiwa kutafunwa na uongozi wa kikundi hicho.
Akiongea na wanahabari jijini hapa moja ya wanakikundi hicho chenye makao makuu eneo la Ngusero kata ya Sombetini jijini hapa Grace Magala alisema kuwa kikundi chao chenye umri wa miaka mitano tangia kuanzishwa kwake, hawakuwahi kugawana faida yoyote hadi juzi walipokaa na kukubaliana kugawana faida.
Alieleza kuwa kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na katibu wa kikundi hicho Deogratius Seif kikundi hicho hadi kuvunjwa juzi kulikuwa na faida ya kiasi cha million 39 ambazo zilipaswa kugawanywa kwa wanakikundi hao lakini katika hali ya sintofahamu wanakikundi hao waliambiwa fedha hizo zimeyeyuka katika mazingira ya kutatanisha jambo lililozua taharuki kwa akina mama waliokuwa wameambatana na waume zao kwa ajili ya  kupokea gawio .
Alisema kuwa siku ya Ijumaa ya wiki ya jana,wanakikundi hao walijikusanya kwenye ukumbi wa shule ya Highview  kwa lengo la kupata gawio la faida ya michango yao ndani ya kikundi lakini walishangaa mhasibu wa kikundi hicho, Halima Mwidadi alipowaeleza kuwa hakuna fedha zozote zaidi ya hizi million 39 kwani mahala alipozihifadhi hazionekani.
Kutokana na mgawanyo huo sisi tulihoji ni kwanini fedha nyingine zipotee zaidi ya milioni 40 wakati nyingine zipo ndani ya sanduku akijibu hilo katibu alisema kuwa fedha nyingine zipo kwa mikononi mwa wanachama hivyo wasubiri mchakato unaendelea.
“Ndugu zangu nilipewa taarifa hizi na mwanachama mwezangu Halima kwitema na kunieleza upotevu wa fedha zetu zimepotea huku wenzetu wakiwa wamezima baada ya kusikia taarifa hiyo tunaiomba serikali kuingila kati suala nhilo kulipatia ufumbuzi”alisema
Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho Deogratius Seif alisema kuwa kimsingi bado wanaendelea na ufuatiliaji wa suala hilo na watakutana viongozi wote wa kikundi  kujua kwa kina ndipo watatoa taarifa kamili kama kuna upotevu wa fedha ama kuna makosa ya  kimahesabu.
Alisema suala hilo hata yeye linamuumiza kichwa hadi muda huu mnaponihoji Napata wakati mgumu kwa kuwa hatujakaa kama viongozi kujua suala zima la upotevu kwani tupo watu sita mimi nilikabidhi taarifa ya mahesabu kwa wananchama nilioandaa ikiwa na kiasi cha milioni 39 badala ya milioni 120.
Akiongelea suala hilo kwa njia ya simu mweka hazina wa kikundi hicho,Halima Mwidadi alisema kuwa bado anaendelea kufanya mahesabu vizuri ili kubaini  kiasi cha fedha kilichopotea ila nakubaliana na upotevu huo ila hajui fedha hizo zimepotea kimazingira au ushirikina kwa kuwa sanduku halijavunjwa sehemu yoyote na kukata simu.
Kwa mujibu wa baadhi ya wanachama wa kikundi hicho  walipendekeza kuwa suala hilo lifikishwe  kwenye vyombo vya dola ili wahusika waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria , hata hivyo wameshangazwa kuona fedha hizo zikihifedhiwa ndani ya nyumba ya mweka hazina huyo  tofauti na makubaliano ya kwamba fedha zote za wanachama zihifadhiwe benki kwa ajili ya usalama zaidi ili kuepusha suala la upotevu.
Wanakikundi hao wanatarajiwa kuketi kesho ili kujua mwafaka wa upotevu wa kiasi nhicho cha fedha zaidi ya milioni 40 zinazodaiwa kutafunwa na mhasibu huyo na wenzake kinyuem cha sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *