Shirika la haki yangu foundation lazinduliwa rasmi, mkurugenzi mhe. salome makamba ataja malengo

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Shirika jipya lisilo la kiserikali la HAKI YANGU FOUNDATION
limezinduliwa rasmi leo katika ukumbi wa African Dreams Mkoani Dodoma na   litajikita katika miradi ya kutetea na
kusaidia wanawake na watoto wenye uhitaji Nchini hasa katika Mkoa wa Shinyanga
kwa kipindi cha miaka mitano.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi muasisi na mkurugenzi
wa shirika hilo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia
CHADEMA, Bi. Salome Makamba ametumia fursa hiyo kubainisha malengo ya shirika
kuwa ni kusaidia jamii katika masuala ya    kisheria, kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Haki Yangu amesema
Mkoa wa Shinyangani moja ya eneo litakalofikiwa sana huku baadhi wa wadau
waliohudhuria uzinduzi huo wakipongeza juhudi hizo.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya shirika la Haki
Yangu Bwana Richard Haule amesema Mkoa wa Shinyanga ni moja ya eneo
litakalofikiwa na ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo  kutoa ushirikiano pindi shirika hilo
litakapowafikia.

Uzinduzi wa Shirika la Haki Yangu umehudhuriwa na
viongozi wa serikali ,vyama vya siasa na wadau mbalimbali huku Mbunge wa viti
maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Felista Njau pamoja na Mbunge wa CCM jimbo la
Kasulu Vijijini Mhe. Vuma Agustine wamepongeza upunifu na hatua aliyoifanya
Mhe. Salome Makamba katika kusaidia na kutetea haki za wanawake na watoto ili
kupunguza au kumaliza kabisa ukatili uliopo katika jamii.

Muasisi na mkurugenzi wa shirika la Haki Yangu
Fondation ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia
CHADEMA, Bi. Salome Makamba akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa shirika
hilo.

Muasisi na mkurugenzi wa shirika la Haki Yangu
Fondation ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia
CHADEMA, Bi. Salome Makamba akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa shirika
hilo.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Grace Victor Tendege akizungumza kwenye uzinduzi wa shirika la Haki Yangu uliofanyika Mkoani Dodoma.Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Grace Victor Tendege akizungumza kwenye uzinduzi wa shirika la Haki Yangu uliofanyika Mkoani Dodoma.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.
Felista Njau akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa shirika la Haki Yangu
Foundation uliofanyika Mkoani Dodoma.

Hafla ya uzinduzi wa shirika la Haki Yangu Foundation ikiendelea katika ukumbi wa African Dreams Mkoani Dodoma.

Muasisi na mkurugenzi wa shirika la Haki Yangu
Fondation ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia
CHADEMA, Bi. Salome Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi
waliohudhuriwa uzinduzi wa shirika hilo.