Shirika la msalaba mwekundu kigoma lakabidhi vifaa vya huduma ya damu na vifaa tiba vyenye thamani ya milion 67

Wa katikati ni Meneja wa mradi wa damu salama Redcross Kigoma akitoa
maelekezo ya matumizi ya vitu vya kulalia wakati wa kuchangia damu kwa
mganga mfawidhi wa mkoa Dkt. Osimundi Dyegula

Wa kwanza kushoto mwenye suti la blue ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Kigoma
Dkt Saimon Chacha akipokea moja ya kifaa kutoka kwa mwenyekiti wa
Redcross Kigoma Musa Kifyumu
Na Diana Rubanguka,  Kigoma.
Shirika
la msalaba mwekundu Tanzania red cross Mkoa wa Kigoma limetoa msaada wa
vifaa tiba vya damu salama vyenye thamani ya zaidi ya shilingi niliona
68 ikiwa ni sehemu ya kuchangia huduma za kijamii katika mradi huo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
mwenyekiti wa shirika la Redcross Mkoa wa Kigoma Musa Kifyumu alisema
shirika hilo lilitembelea vituo vya damu ya kibaoni changamoto
mbalimbali ambazo nimekua chachu ya kutoa vifaa hivyo.
“tulibaini
ukosefu wa vitu vya kulalia wakati wa kuchangia damu, vifaa vya
kuhifadhia damu, elimu kwa watoe huduma pamoja na umeme wa dharula hivyo
tukaona tuchangie katika changamoto hizo” alisema kifyumu.
Mganga
MKuu wa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Kigoma Dkt. Saimon Chacha alishukuru
shirika hilo kwa kutambua changamoto hizo za vituo vya damu na
kuzifanyia kazi.
Dkt.
Chacha alitoa wito kwa watumishi wa afya kuthamini na kutunza mchango
huo kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya kutotunza na kujali vifaa
vinavyotolewa na wadau kwa kutovinea uchungu.
Hata
hivyo ameiomba Redcross kushirikiana na serikali katika kutoa huduma
itakapohitajika  kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Korona katika nchi
mbalimbali ambapo Tanzania sio hawanga lakini shirika la World Health
organisation WHO limethibitisha uwepo wa mgonjwa mmoja nchini Kongo nchi
ambayo ni jirani na Mkoa wa Kigoma kwa kuwa muingiliano wa shughuli za 
kiuchumi ni mkubwa hivyo lolote linaweza kutokea.
Awali
Meneja mradi wa damu salama Redcross Kigoma Abich Maramba alivitaja
vifaa hivyo kuwa ni jokofu la kuhifadhia damu, vitanda 16 vya kulalia
wakati wa kuchangia damu, vibebeo 8 vya sampuli ya damu, vibebeo 10 vya
damu, Mizani mitatu ya kupima damu na mmoja wa kupima uzito. 
Sambamba
na hivyo wametoa computa mpakato moja, printa, computa ya mezani, Viti
vya ofisini vitano, jenerata kubwa la umeme pamoja, vitanda viwili vya
kulalia wakati wa kuchangia damu pamoja na box la vifaa vya maabara vya
dharula.