Shirika la nyumba la taifa mkoani arusha lakabidhi mifuko 100 ya saruji shule ya sekondari felix mrema

Kushoto Ni meneja wa shirika la nyumba la Taifa mkoani Arusha, Ladislaus Bamanyisa akimkabithi mifuko Mia moja ya saruji  Jana mkuu wa shule ya sekondari Felix Mrema ,Reginaldo Msendekwa aliyepo kulia katikati ni Mwenyekiti wa mtaa wa Jamhuri , Hussein Dudu ,ambapo mifuko hiyo ya saruji  itasaidia ukarabati wa sakafu iliyochakaa
Mkuu wa shule ya sekondari Felix Mrema Reginaldo  Msendekwa akimuonyesha Meneja wa shirika la nyumba , Ladislaus Bamanyisa aliyeko kushoto moja ya vioo vilivyowekwa hivi karibuni shuleni hapo baada ya shirika Hilo kutoa kiasi Cha shs 2 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vioo vipya vya madirisha hayo kutokana na yaliyokuwepo kupasukaNa Ahmed Mahmoud,Arusha

Arusha.Shirika la nyumba la Taifa (NHC)mkoani Arusha limekabithi msaada wa mifuko 100 ya saruji  yenye dhamani ya shs 1.7milioni kwa shule ya sekondari Felix Mrema iliyopo kata ya Daraja mbili kwa ajili ya ukarabati wa sakafu za madarasa .

Akizungumza wakati wa kukabithi msaada huo,Meneja wa shirika la nyumba mkoani Arusha , Ladislaus Bamanyisa alisema kuwa msaada huo ameutoa kutokana na ahadi aliyoahidi mwaka Jana shuleni  hapo wakati akiwa mgenirasmi katika mahafali na kujionea uchakavu wa sakafu katika madarasa mbalimbali.
Alisema kuwa,shirika hilo limefikia hatua ya kutoa msaada huo ikiwa ni malengo waliyojiwekea ya kurudisha kiasi cha faida wanachokipata kwa jamii .
Bamanyisa alisema  kuwa,shule hiyo  imejengwa muda mrefu na hivyo kusababaisha miundombinu mingi kuwa mibovu ikiwemo sakafu,vyoo pamoja na vioo vya madirisha kupasuka.
Alifafanua kuwa ,shirika hilo liliwahi kukabithi kiasi Cha shs 2 milioni kwa shule hiyo ambazo zimesaidia kukarabati vioo vya madirisha kwa kuweka vingine kutokana na vile vilivyokuwepo kupasuka muda mrefu.
“mifuko hii ya saruji itasaidia Sana kukarabati sakafu za  madarasa zilizochakaa kwa muda sasa,na tunaahidi kuendelea kusaidia zaidi kwani kwa kufanya hivi tunamuunga mkono Rais wetu katika kuboresha elimu kwa watoto wetu ,”alisema Meneja.
Aidha alitoa wito kwa taasisi zingine pamoja na mashirika mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangia elimu hususani katika shule ya sekondari Daraja mbili kwani kwa kufanya hivyo Ni njia mojawapo ya kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuboresha huduma ya elimu.
Naye mkuu wa shule hiyo, Reginaldo Msendekwa alishukuru shirika la nyumba  mkoani Arusha  kwa msaada huo ambao shirika liliahidi mwaka Jana ambapo utaweza kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya uchakavu wa sakafu uliopo katika madarasa mengi.
Msendekwa alisema kuwa, shirika hilo mbali na kukabithi mifuko hiyo ya saruji pia walishawakabithi   kiasi Cha shs 2 milioni kwa ajili ya ukarabati wa vioo vya madirisha ambavyo tayari vilishakarabatiwa .
Aidha alitoa wito kwa wadau mbalimbali pamoja na mashirika kujitokeza kusaidia elimu ya vijana wetu , kwani ndio wanaotegemewa katika kuwa nguvu kazi katika viwanda vyetu .
Naye mjumbe wa  bodi  ya shule hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Jamhuri ,Hussein Dudu alishukuru Sana shirika hilo kwani msaada huo utasaidia Sana kuboresha miundombinu ya shule hiyo hususani ukarabati wa sakafu za madarasa ambazo zilikuwa zimechakaa kwa muda mrefu Sana pamoja na ukarabati wa matundu ya vyoo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *