Shirika la tcrs kwa ufadhili wa nca yafungwa wilaya ya kishapu washiriki wakumbushwa kuendeleza ujuzi

Na Mapuli Kitina Misalaba

Shirika
la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) kwa ufadhili wa kifedha kutoka
shirika la Norwegian Church Aid (NCA); limeendesha mafunzo yakuongeza thamani
kwenye mazao hasa Nyanya, kwa wakulima pamoja na wadau wengine wa kilimo kutoka
kata za Sekebugolo na Mondo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

 Mafunzo
hayo yamefanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano kijiji cha Mwigumbi
Wilaya ya Kishapu na kwamba yameandaliwa na shirika la TCRS huku wawezeshaji
wakitoka  shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga.

Wakulima
20 walioshiriki mafunzo hayo wamepewa vyeti wakiwemo wafanyabiashara wa zao la
Nyanya kutoka kwenye vijiji vinne ambavyo ni Mipa, Dulisi, Weshiteleja pamoja
na kijiji cha Sekeididi na kwamba wamepewa mafunzo mbalimbali ikiwemo 
usindikaji wa zao la nyanya ili kupata  Tomato Sauce and Tomato 
Paste.

 Akizungumza
kwenye mafunzo hayo afisa uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia
viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban amewasisitiza washiriki
baada ya kupata elimu hiyo, kujiendeleza zaidi na ujuzi huo ili waweze 
kunufaika wao na jamii kwa ujumla.

“Baada
ya mafunzo haya na leo hii tumetunukiwa vyeti yasiishie hapa hapa ni lazima
tuhakikishe kwamba ujuzi huu tulioupata ukawe na manufaa kwetu na watu wengine
wanaotuzunguka, hapa umepata ujuzi lakini ili uweze kuwa na manufaa, ujuzi huu
ni wewe kuendelea kufanyia mazoezi hata kabla hujaanza kuanzisha hicho kiwanda
kidogo cha usindikaji anza kusindika kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani kwanza
halafu badaye utakavyokuwa unafanya mara kwa mara utakuwa unagundua na vitu
vingine ambavyo hukujifunza awali”.
amesema Taban

 

Kwa
upande wake afisa uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka SIDO  Bwana Abel
Bebwa amewasihi washiriki hao kujiamini zaidi kwenye utekelezaji wa majukumu
yao ikiwemo kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika Maisha ya kila siku.

 Naye
afisa Kilimo kutoka shirika la TCRS Wilaya ya Shinyanga Bwana Laurent Stanslaus
amezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo hasa kwa wakulima na wafanyabiashara wa
zao la Nyanya.

“Mafunzo
haya yanalenga hasa kuweza kupunguza matatizo ambayo yanatokana na uharibifu wa
chakula kwa sababu kuna muda wakulima wanavuna mazao mengi hasa mazao
yanayowahi kuharibika mfano zao la Nyanya akivuna halafu unakuta soko ni
changamoto kwahiyo tumeona kwamba tuwape mafunzo haya ili mkulima aweze kuwa na
uwezo wa kufaidika na mazao anayoyapata”.
amesema Stanslaus

 Washiriki
wa  mafunzo hayo wameshukuru TCRS, NCA pamoja na shirika la SIDO kwa
kuwapa elimu hiyo ambayo wamesema itawasaidia kuinuka kiuchumi hasa katika
Biashara pamoja na shughuli zingine za kwenye familia zao ikiwemo kusomesha
watoto.

 

Afisa
uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO 
Bwana Abel Bebwa akitoa maelekezo kwa washiriki wa mafunzo hayo kuhusu mambo
muhimu ya kuzingatia katika usindikaji wa sosi ya Nyanya. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *