Shule 10 bora kitaifa,mikoa 10 iliyoongoza,watahiniwa 10 bora kitaifa matokeo darasa la saba 2019Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo
asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku
watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo
Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya
wavulana waliofanya vizuri zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa
ya kanda ya ziwa.


Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne
Oktoba 15, 2019 Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa
jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 lakini ufaulu
katika somo la Kiingereza bado ni mdogo likilinganishwa na masomo
mengine.


“Ufaulu katika somo la Kiingereza
unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi
zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika
somo hili,” amesema Dk Msonde.


Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori
Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa
kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise
ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya
msingi Mbezi ya Dar es Salaam.


Wengine katika orodha ya 10 bora ni
Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki
goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little
Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele
wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.


Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya
Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya
Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya
Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya
Shinyanga.


Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika
namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro,
Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.


Halmashauri 10 bora zimeongozwa na
Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi
Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha