Smaujata mkoa wa shinyanga wakutana na kuzungumza na askofu sangu wa kanisa katoliki jimbo la shinyanga

Askofu wa Kanisa katoliki
Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akizungumza na viongozi wa kampeni
ya kupinga ukatili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga.

Na
Mapuli Kitina Misalaba

Askofu wa Kanisa katoliki
Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amesema jukumu la kulinda maadili
ya jamii linahitaji ushirikiano wa dhati kuanzia hatua ya malezi na makuzi ya
Mtoto  katika ngazi ya familia.

Ameyasema hayo  wakati akizungumza na Viongozi wa kampeini ya
kupinga ukatili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga walipomtembelea jimboni kwa lengo la
kumpongeza kutokana na juhudi zake katika mapambano ya kupinga ukatili.

Askofu Sangu amesisitiza
kuhusu Msingi na umuhimu  wa Elimu ya
ukatili  kuanzia  kwenye ngazi ya familia ili kujenga jamii
yenye maadili mema.

“Sisi
sote kwa pamoja tuendelee kushirikiana katika kujenga jamii yenye maadili
mema  lakini hii Elimu ya ukatili dhidi
ya binadamu lazima ishuke iende kwenye Familia, Familia ndiyo shule baadhi ya
Familia watoto wanakua hawalelewi yaani Mama anamuacha mtoto kwenye kisenta
anaenda kufanya kazi zake sasa yule mtoto analelewaje anafundishwa maadili ya
namna gani kwa sababu mtoto kuanzia Mwaka mmoja hadi Miaka saba lazima awe
karibu na wazazi kumbe tunapopeleka watoto kwenye Baby care asilimia 85 ya
mtoto ni ya yule siyo yako tena mzazi ndiyo maana tabia mbalimbali sana zinaibuka”amesema
Askofu Sangu

Amesema Kanisa litaendelea kushirikiana na serikali
pamoja na wadau wote katika juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia kwa
kumshirikisha mwenyezi Mungu

Ametumia nafasi hiyo pia kuipongeza kampeni ya
SMAUJATA kwa kuguswa kujitolea katika kupambana na ukatili wa kijinsia  huku akiwakumbusha kuendelea kumtanguliza
Mungu

“Nimethamini
wito wenu na kile mnachokifanya kwa ajili ya jamii sote tuko pamoja katika
kupambana na hili janga kubwa la ukatili lakini ukatili umekuwa mbaya zaidi kwa
sababu uko ndani ya Familia kama ni Shetani ameingia ndani kabisa kwenye
chimbuko la maisha la ustawi wa jamii na kwa nini ukatili upo kwa sababu
binadamu hathamini utu wa mtu mwenzake tunaposahau hii kwamba binadamu ameumbwa
kwa sura ya mfano wa Mungu tunapotea kabisa maadili yanapotea”

“Kumbe
kwenye kampeni hii tuko pamoja nawaalikieni katika Kanisa letu njooni kuna
makongamano ya vijana njooni, semina za vijana njooni, vigangoni kwenye
Parokiani njooni, Radio Faraja iko hapo tumieni Radio lakini tunawakaribisheni
katika ngazi zote”.

“Kwahiyo
basi tutaendelea kushirikiana lakini tukumbuke yote yanawezekana katika yule
atutiaye nguvu  pamoja na kampeni yetu
hii ya SMAUJATA tumtangulize zaidi Mungu pamoja na kufanya juhudi zetu zote za
huku na huku tujue kwamba bila Mungu hatuwezi chochote kumbe tuikabidhi yote
mkononi mwa Mungu”.
amesema Askofu Sangu

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa
wa Shinyanga, Mwenyekiti idara ya Itifaki, uanachama na uenezi Bwana Solomon
Najulwa amelipongeza Kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga kwa juhudi zake
mbalimbali za kupinga ukatili.

 “SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga inalipongeza sana
Kanisa Katoliki lakini pia kwa usimamizi wako mzuri sana Baba Askogu Liberatus
T.K Sangu kwa jinsi ambavyo Kanisa limeendelea kupinga ukatili katika mahubiri
na makongamano mbalimbali ambapo sisi SMAUJATA huwa tunafuatilia sana tukijua
kwamba Kanisa liko pamoja na SMAUJATA kwahiyo nirudie kwa kusema kwamba Baba
Askofu Mungu akubariki sana wewe pamoja na uzao wako na Kanisa kwa ujumla mpate
kubarikiwa siku zote”.
amesema Najulwa

Kwa upande wake Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
Bwana Daniel Kapaya naye ametumia nafasi hiyo kumpongeza na kumshukuru Askofu
Sangu kwa kuendelea kutekeleza vema utume wake.

“Jambo
la msingi kuja katika eneo hili Baba Askogu kwanza kabisa ni kukupongeza na
kukushukuru kwa kufanya kazi kubwa sana ya kupinga ukatili umekuwa ukizungumza
katika mahubiri yako ambayo tunayafuatilia sana lakini vile vile tunasikia
katika vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na Radio Faraja unakemea sana vitendo
vya ukatili”.
amesema Kapaya

Viongozi wengine wa kampeni hiyo akiwemo Mwenyekiti
wa idara ya Utamaduni, mila na destori Mwinjilisti Esther Emmanuel, Mwenyekiti
wa idara ya uhitaji, maafa na makundi maalum Mhandisi Peter Mangula, Mwenyekiti
idara ya jinsia Ispekta Alkwin Willa, pamoja na Mwenyekiti idara ya Elimu
(Wanafunzi, Vyuo na Vyuo vikuu) Mwalimu leonard Mapolu wamepongeza huku
wakiahidi kutekeleza majukumu yao kwa haki za usawa kwa lengo la kutokomeza
ukatili wa kijinsia Mkoa wa Shinyanga.

Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania
(SMAUJATA) ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini ambayo inatekeleza majukumu yake
chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

Kampeni hiyo ipo Mikoa yote na kwamba imeanzishwa na
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Shujaa Sospeter Bulugu kwa kushirikiana na Waziri
wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima
kwa lengo la kushirikiana na Serikali katika kupinga vitendo vyote vya ukatili
Nchini.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga, Mwenyekiti idara ya Itifaki, uanachama na uenezi Bwana Solomon
Najulwa amelipongeza Kanisa katoliki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *