Smaujata mkoa wa shinyanga yawakumbusha viongozi na wadau wa kupinga ukatili kukemea rushwa

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga
Bi. Nabila Kisendi amewakumbusha viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa kupinga
ukatili kuendelea kukemea rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameyasema hayo wakati
akizungumza na viongozi wa SMAUJATA Wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo
amesisitiza viongozi hayo kutojihusisha na 
rushwa katika utetezi wa haki za wahanga wa ukatili na uhalifu
unaoendelea kufanyika kwenye jamii.

Mwenyekiti huyu Nabila
Kisendi pamoja na mambo mengine amewahimiza viongozi wa SMAUJATA kuwa mabalozi
wazuri wa kupambana na ukatili huku akiwasisitiza kupambana na rushwa ili hatua
za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi ya wahalifu.

Mwenyekiti idara ya
maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) amesema ni
muhimu viongozi kuwa waadilifu katika kupambana na rushwa.

Kwa upande wake katibu
wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya ameiomba serikali kupitia
mamlaka husika kuendelea kuchukua hatua kali kwa watu wanaobainika kujihusisha
na rushwa ili kutokomeza vitendo hivyo.

Baadhi ya viongozi
Wilaya ya Shinyanga vijijini wameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na
taratibu zilizopo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali katika
kupambana na ukatili.

SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga imefanya ziara ya siku moja Wilaya ya Shinyanga vijijini kwa lengo la
kuimarisha viongozi ngazi ya Wilaya.

Mwenyekiti wa kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga
Bi. Nabila Kisendi akiwasihi viongozi kuepuka rushwa katika utekelezaji wa
majukumu yao.

Mwenyekiti wa kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga
Bi. Nabila Kisendi akiwasihi viongozi kuepuka rushwa katika utekelezaji wa
majukumu yao.

Katibu wa kampeni ya
shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bwana
Daniel Kapaya akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti idara ya
maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) akizungumza
kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti idara ya Michezo
 SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni
Polisi wa kata ya Ndala afande Alkwin Willa akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya
Shinyanga Stella Gershom
akizungumza kwenye
kikao hicho.

Katibu wa SMAUJATA Manispaa ya
Shinyanga Hasna Maige 
akizungumza kwenye
kikao hicho.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya
Shinyanga vijijini Bwana Emmanuel Makolo 
akizungumza
kwenye kikao hicho.

Kikao cha viongozi wa SMAUJATA ngazi ya Mkoa pamoja
na viongozi ngazi ya Wilaya ya Shinyanga vijijini kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa SMAUJATA ngazi ya Mkoa pamoja
na viongozi ngazi ya Wilaya ya Shinyanga vijijini kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa SMAUJATA ngazi ya Mkoa pamoja
na viongozi ngazi ya Wilaya ya Shinyanga vijijini kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa SMAUJATA ngazi ya Mkoa pamoja
na viongozi ngazi ya Wilaya ya Shinyanga vijijini kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa SMAUJATA ngazi ya Mkoa pamoja
na viongozi ngazi ya Wilaya ya Shinyanga vijijini kikiendelea.

Mwenyekiti wa kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga
Bi. Nabila Kisendi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Mwenyekiti wa kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga
Bi. Nabila Kisendi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.