Spika ndugai ataka hatua za haraka zichukuliwe kusaidia waathirika wa mafuriko lindi

Mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali zimesababisha maafa
makubwa ikiwemo watu wanne kupoteza maisha na watu zaidi ya 661 katika
vijiji zaidi ya sita wakikosa makazi ya kuishi katika mikoa ya Lindi na
Iringa.


Pamoja na hayo, miundombinu ikiwemo madaraja na mashamba imeharibiwa vibaya na mvua hizo.

Mkoani
Lindi watu 600 kutoka vijiji vya Mikole, Kipindimbi, Makanganga Mitolea
wilayani Kilwa jana wameokolewa kwa njia ya boti baada ya kuzungukwa na
maji yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha.

Leo
January 28, 2019  Spika wa Bunge, Job Ndugai amezungumzia hali ya
mafuriko hayo hasa mkoani Lindi na kutaka ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) kuchukua hatua
za haraka katika kusaidia waathirika wa mafuriko hayo ambayo
yamesababisha vifo vya watu nane hadi sasa.


“Ni kweli mvua inanyesha karibu kila mahali nchi nzima lakini kwa
taarifa tulizo nazo hivi sasa ni kwamba katika Mkoa wa Lindi katika
jimbo la Waziri Mkuu kule Luangwa kuna mafuriko kwahiyo tunakuomba sana
Waziri wa nchi uweze kuona hali hiyo,” – Amesema Spika wa Bunge, Job
Ndugai leo Bungeni