Taarifa kwa umma kutoka jeshi la polisi mkoani mwanza

Jeshi
La Polisi Mkoa Wa Mwanza  Limefanikiwa Kuipata Silaha Moja Aina Ya
Bastola Ikiwa Na Risasi Tatu  Zinatumiwa Na Wahalifu (Majambazi) Kwenye
Matukio Mbalimbali Kanda Ya Ziwa  Baada Ya Watuhumiwa Wawili Wa Ujambazi
Wanaume  Ambao Bado Hawajafamika Majina Wala Makazi Yao Wanaokadiriwa
Kuwa Na Umri Kati Ya  Miaka 25 Hadi 30 kufariki.


Watuhumiwa
Hao Walifariki Wakati Wakipelekwa Hospitali Baada Ya Majibizano Ya
Kurushiana Risasi Na Askari Polisi Baada Ya Kumtishia Kumuua  Kwa
Bunduki Na Baadae Kupora Pikipiki Ya ” Mwendesha Bodaboda “.

Tukio
Hilo Limetokea Tarehe 26.11.2019 Majira Ya  23:40hrs Huko Maeneo Ya
Sweya – Fisheries Wilayani Nyamagana, Hii Ni Baada Ya Mwendesha Pikipiki
Samwel Masanja (Bodaboda)   Kuporwa Pikipiki Yake Maeneo Ya Maina Na
Watu Hao  Na Baadae Wananchi Kutoa Taarifa Polisi.

Baada
Ya Kupatikana Kwa Taarifa Hizo Askari  Polisi (Makachero) Walifanya
Ufuatiliaji Wa Haraka Na Baadae Wakakutana Na Wahalifu  Hao Uso Kwa Uso
Maeneo Ya Sweya, Walipobaini Kufuatiliwa Walianza Kuwarushia Risasi
Askari  Na Askari Walijihami Na Kufanikiwa Kuwajeruhi Kwa Risasi
Wahalifu Hao Ambao Baadae Walifariki Dunia  Wakati Wakipatiwa Matibabu
Hospitali Ya Bugando.

Katika
Eneo La Tukio Kumepatikana Bastola Moja Aina Ya Starbird Yenye Namba Za
Usajili Us Patten 2563720 Pamoja Na Risasi Tatu Ndani Ya Magazine Na
Pikipiki Aina Ya San Lg Nyekundu Yenye Namba Za Usajili Mc 617 Abx
Ambayo Ilikua Imeporwa. Imepatikana  Miili Ya Marehemu Wote Wawili
Imehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Ya Bugando Kusubiri Utambuzi Na
Uchunguzi Wa Daktari.

Tukio La Pili.

Tarehe
26.11.2019 Majira Ya 00:05hrs Usiku Huko Maeneo Ya Kifua Wazi Barabara
Kuu Ya Airport –mwanza, Kata Ya Nyamanoro, Wilaya Ya Ilemela, Jiji Na
Mkoa Wa Mwanza. Abiria Mmoja Mwanamke Ambae Bado Hajafahamika Jina Wala
Makazi, Anayekadiriwa Kuwa Na Umri Kati Ya Miaka 25 Hadi 30, Akiwa
Amebebwa Kwenye Pikipiki Yenye Namba Za Usajili Mc 269 Bdy Aina Ya Sanya
Iliyokuwa Ikiendeshwa Na Dereva Aitwaye Novart Joseph, Miaka 26, Mhaya,
Mkazi Wa Jiwe Kuu – Kitangiri, Alianguka Chini Toka Kwenye Pikipiki Na
Kuburuzwa Umbali Kiasi  Cha Mita 70 Baada Ya Mtandio Aliokua Amejifunga
Shingoni Kuingia Na Kujisokota Kwenye Tairi (Spockert) Na Baadae
Kufariki Baada Ya  Kukimbizwa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Sekou Toure Kwa
Ajili Ya Kupatiwa Matibabu. Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Hospitalini
Hapo Kwa Ajili Ya Utambuzi Na Uchunguzi Zaidi Wa Kitaalamu. Dereva Wa
Pikipiki Anashikiliwa Kwa Mahojiano Pamoja Na Pikipiki Hiyo.

Jeshi
La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawashukuru Wananchi Kwa Kuendelea Kutoa
Ushirikiano Katika Kuzuia Na Kupambana Na Uhalifu Na Wahalifu. Pia
Linaendelea Kuwasihi Wananchi Wakati Wote Kuendelea Kutoa Taarifa Za
Uhalifu Na Wahalifu Kwa Jeshi La Polisi Na Linawahakikishia
Kushughulikia Taarifa Hizo Kwa Kuzingatia Weledi Wa Hali Ya Juu.

Aidha
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Abiria Na Madereva Wa Vyombo
Vya Moto Kuzingatia Sheria Za Usalama Barabarani, Hasa Waendesha
Pikipiki Na Wapanda Pikipiki Wazingatie Kuvaa Kofia Ngumu Na Mavazi
Ambayo Hayataleta Madhara Kwa Maisha Yao Ili Kuepusha Vifo Na Majeraha
Yanayoweza Kuepukika.

Imetolewa Na

Muliro J. Muliro –ACP

Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza

27 November,2019