Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, akitunukiwa Tuzo ya Shukrani kutoka kwa viongozi na wanachama wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kwa mchango wake aliotukuka kwenye kuleta mageuzi katika sekta ya habari nchini.
a.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiongoza kikao kazi cha Maafisa
Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini Jijini Mbeya, kushoto ni Naibu wake
Dkt. Ally Possi, kulia ni Katibu
Mkuu -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe
Na John Mapepele, Mbeya
Katibu Mkuu wa Habari wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ametunukiwa
tuzo na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa kutambua
mchango na mageuzi makubwa aliyoyafanya kwenye Sekta ya Habari hapa nchini.
Akikabidhi tuzo hiyo kwa
Dkt. Hassan Abbasi, Mwenyekiti wa TAGCO, Paschal Shelutete wakati wa kikao cha 16
cha TAGCO kilichofanyika Jijini Mbeya Mei 24,2021 amesema Dkt. Abbasi ametoa
mchango mkubwa akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Mkuu wa Serikali
tofauti na hapo awali.
“Ni katika kipindi hiki
ambapo miradi ya kimkakati ya Serikali ilisemewa vizuri zaidi na kufahamika na
watu wengi hivyo kuwafanya wananchi kuipenda Serikali yao” Amefafanua Shelutete.
Ameongeza kwamba Dkt. Abbasi
amefanikiwa kusimamia tasnia ya Habari na uboresha mahusiano ya kikazi miongoni
mwa wadau wote wa Sekta ya Habari.
kwa upande wake Dkt. Abbasi
amewashukuru Waandishi kwa kumpa tuzo hiyo na kuahidi kuendelea kuwapa
ushirikiano ili waweze kuendelea kutekeleza majukumu wao kikamilifu kwa nafasi
yake ya sasa ya Katibu Mkuu. Wizara ya Habari, Utamadunim Sanaa na Michezo.
“Tuendelee kushirikiana
katika cheo hiki kipya cha Katibu Mkuu katika Wizara yetu ambayo ni Wizara
muhimu inayogusa umma kwa nyanja ya burudani na huzuni kutokana na Sekta zake” Ameongeza
Dkt. Abbasi.
Amewataka Waandishi
kuzingatia weledi wakati wote wa undaji wao wa kazi ambapo amesisitiza
kwamba Serikali inatambua mchango wa waandishi na kwamba itaendelea
kuhakikisha sekta inaboreka na
kuchangia kwenye uchumi wa Taifa.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini na kumrejesha tena kwenye nafasi ya Katibu Mkuu na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na bidi ili kutekelea Ilani ya Chama cha
Mapinduzi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia.
Kikao hiki kimefunguliwa na Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa kimehudhuriwa na
Naibu wa Wizara hiyo, Katibu Mkuu -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ambaye ametoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi kwa maafisa Habari kutoka
halmashauri zote nchini,na viongozi mbalimbali wa Serikali na Maafisa
Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa
Serikali zaidi ya 270.