Takukuru geita yawakamata viongozi wa amcos waliotafuna fedha za wakulima

NA SALVATORY NTANDU

Taasisi
ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani wa Geita
imefanikiwa  kurejesha shilingi milioni 23 kati ya 49 zilizokuwa
zimeibwa na baadhi ya  viongozi wa vyama vya Ushiriaka (AMCOS) 8 katika
wilaya Mbogwe.


Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita, Leonidas
Felix katika hafla maalumu ya kukabidhi shilingi milioni 15 kwa
wakulima wa chama cha ushirika Mwanza madaso zilizorudishwa na baadhi ya
viongozi wa AMCOMS hizo.
Amesema TAKUKURU iliendesha zoezi la ukaguzi katika AMCOS zote katika
mkoa wa Geita na kubaini baadhi ya viongozi wake kutumia fedha za
wakulima wa zao la pamba kujinufaisha wao na kutowalipa kwa kuwahadaa
kuwa kampuni za ununuzi bado hazijalipa licha ya kuwa wao tayari
wameshalipwa.
“Mpaka sasa tunawashikilia viongozi 22 wa AMCOS mbalimbali katika mkoa
wetu ambao wameiba fedha za wakulima tumewapa wiki mmoja tuu kurejesha
fedha hizo wengine tayari wameanza kutiii agizo hili na kurejesha
shilingi milioni 23”alisema Felix.
Amefafanua kuwa katika zoezi la ufuatiliaji wa madeni ya wakulima wa zao
la pamba katika mkoa huo wamebaini baadhi ya kampuni za ununuzi wa zao
la pamba kutowalipa wakulima ambapo katika halmashauri ya wilaya ya 
Geita wakulima wanadai zaidi ya shilingi bilioni 1 ambazo wanapaswa
kuzilipa kwa muda wa wiki mmoja ili kuwawezesha kujiandaa na msimu mpya
wa kilimo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Mbogwe,  Matha Mkupas  amewataka
viongozi wa AMCOS kwa kushirikiana na Maafisa Ushirika kuhakikisha
wakulima wanalipa madeni ya pembejeo ya msimu uliopita kabla ya kulipwa
fedha zao  baada ya kampuni za ununuzi wa pamba kuwalipa.
“serikali ya awamu ya Tano haiwezi kukubali wakulima wake kuendelea
kunyanyaswa na viongozi wa AMCOS ambao ni wabadhilifu wanaowaibia
wakulima tutahakikisha tunawakamata wote hadi walipe fedha za
wakulima”alisema Mkupas.
Nao baadhi ya wakulima wa Zao la Pamba katika AMCOS ya Mwanza Madaso,
Suzana Nkinjiwa na Rafael Shizya wamesema kucheleweshwa kwa malipo ya
zao hilo kwa msimu huu yatasababisha kushuka kwa uzalishaji kutokana na
wakulima wengi kukata tamaa