Tamasha la maonyesho ya utamaduni wa kisukuma kufanyika tena nhelegani mwezi ujao

Tamasha hili litafanyika tarehe 8 hadi tarehe  9 ya mwezi wa saba (7) 2023, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nhelegani, kushiriki katika mabanda ya maonyesho piga simu 0712583756.

Wizara imetoa ushirikiano wa dhati kabisa kupitia kampuni ya The BSL Investment Company Limited inayomilikiwa na Mr. Black. Ikumbukwe kwamba Tamasha hili linakwenda kufanyika kwa mara ya pili mara baada ya mwaka jana 2022 kuhudhuriwa na zaidi ya watu 3000.
 Tamasha hili hubeba maudhui ya maonyesho ya utamaduni wakisukuma kama vile ngoma za asili, michezo ya fisi, Nyoka, mbio za baiskeli, maonyesho ya mavazi ya kisukuma, vyakula na vinywaji vya asili. 

Tamasha hili hupambwa na kuandaliwa vyema kabisa kupitia waandaaji hawa wenye uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha ya aina mbalimbali, Mwaka huu Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, mabalozi wa Nchi mbalimbali, viongozi mbalimbali ngazi ya wizara, mkoa na wilaya.

Tamasha hili litahusisha maonyesho ya biashara na huduma mbalimbali kupitia makampuni, taasisi za umma na binafsi, wajasiriamali na vikundi mbalimbali vya sanaa za utamaduni pia ma chief wa utamaduni wa kisukuma.

Ikumbukwe kuwa tamasha hili halina kiingilio kwa watazamaji wote, Hivyo watanzania wote mnakaribishwa kupata burudani bila kukosa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “TUENZI MILA NA TAMADUNI ZETU, PINGA UKATILI WA KIJINSIA”. 

Hakika hii ni zaidi ya siku kuu kwa wasukuma wote nasi tunasema SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL …LEJIGUKULU LYA NZENGOOOO 

kushiriki katika mabanda ya maonyesho piga simu 0712583756.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma (Mwana FA) na  Mwandaaji wa Tamasha la Utamaduni wa Msukuma (SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL) Mr. Peter Frank alimaarufu Mr. Black upande wa kulia baada ya mazungumzo ya maandalizi kamili ya Tamasha hili litakalofanyika tarehe 8 na 9 ya mwezi wa saba 2023, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nhelegani.