Tanesco yashiriki maonyesho ya utalii na biashara chato

 

Meneja
wa Wilaya ya Chato Bw.Nyaonge Nyabinyiri akitoa maelezo kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe mara baada ya
kutembelea banda la TANESCO wakati wa maonesho ya Utalii na Biashara
yanayofanyika Chato.

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa katika banda lao wakati wa maonesho ya Utalii na Biashara yanayofanyika Chato.

Muonekano wa Banda la TANESCO katika Maonesho ya Utalii na Biashara yanayofanyika Chato.

Shirika
la Umeme nchini (TANESCO) limeshiriki katika maonesho ya Utalii na
Biashara Chato ikiwa ni mdau muhimu kwenye kuvutia uwekezaji Chato.

Maonesho
hayo yameanza Agosti 7, mwaka na kufunguliwa leo Agosti, 11,2021 na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe.

Shirika hilo limewahakikishia wananchi na wafanyabiashara uhakika wa umeme wa kutosha ili kuwekeza wilayani Chato Mkoani Geita.

Katika
banda la TANESCO wananchi wanaweza kujionea kifaa cha UMETA ,ambacho
wataalamu wanaonyesha hatua zote kuanzia maombi ya umeme hadi hatua ya
mwisho umeme unapomfikia mteja.

Pia wananchi wamelisifu Shirika hilo kwa hali ya upatikanaji umeme kwa hivi sasa.

“Kwa
kweli mnastahili pongezi, tulikuwa katika shida kubwa ya kupata umeme
wa uhakika kwa muda mrefu, lakini hali kwa sasa imebadilika sana, umeme
hausumbui kama ilivyokuwa hapo awali.” wamesema wananchi

Kilele cha maonesho hayo kitakuwa Agosti, 15 mwaka huu