Tanga uwasa wakabidhi madawati 50 kwa shule ya msingi saruji jijini tanga.

 

MKUU
wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akikata utepe kuashiria kupokea
madawati 50 kwenye shule ya Msingi Saruji yaliyotolewa na Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) leo kulia ni Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Jiji la Tanga Mwalimu Lilian Kihama


MKUU
wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati aliye vaa suti akiwa
amekaa kwenye moja ya madawati 50 yaliyotolewa na Tanga Uwasa mara
baada ya kuyapokea


MKUU
wa wilayaya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza mara baada ya kupokea
madawati hayo kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi
Ahmad kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu Lilian Kihama
na Diwani wa Kata ya Maweni Colvas


Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad akitoa hotuba yake wakati wa
halfa hiyo ya makabadhiano kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa

Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu Lilian kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga
Uwasa Alawi Ahmad kulia ni Diwani wa Kata ya Maweni Colvas Joseph

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Saruji Hellen Makange  akisoma taarifa ya shule hiyo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Saruji wakiwa wamekalia madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa leo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Saruji wakiwa wamekalia madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa leo

Mkurugenzi
wa Tanga
Uwasa Alawi Ahmad akipokea cheti cha shukrani kutokana na Msaada huo wa
madawati kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa ajili
ya kutambua mchango mamlaka hiyo kusaidia sekta ya elimu kulia ni
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu LilianMKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo

Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa ya makabidhiano hayo.

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga  (Tanga
UWASA) leo wamekabidhi msaada wa madawati katika shule ya Msingi Saruji
Jijini Tanga na kuwasaidia kuondoa adha ya wanafunzi wa shule hiyo kukaa
chini.

Makabidhiano
hayo
yalifanyika  shuleni hapo na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Tanga
Uwasa  Alawi Ahmad Meneja  (kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji)  kwa Mkuu
wa wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa.

Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga
Uwasa Alawi Ahmad alisema Mamlaka hiyo leo wanatoa msaada wa madawati 50
kwa shule ya Msingi Saruji iliyopo Kata ya Maweni wenye thamani ya
Milioni 4.5.

Awali Meneja
huyo wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa alisema mchango huo wa madawati
ni mwendelezo katika utekelezaji wa mpango wa Mamlaka wa kuchangia sekta
ya elimu kwa kuangalia maeneo yenye mahitaji.

Alisema
msaada huo ni hatua mojawapo ya Mamlaka hiyo kuunga mkono juhudi za
Serikali inayoongozwa na  Rais Dkt John Magufuli katika kutoa elimu
bure.

Alisema wanategemea madawati hayo yatatumiwa vizuri na kutunzwa ili yaweze kuwanufaisha watoto wengi kwa miaka mingi.

 “Tunapenda
kuishukuru Serikali ya wilaya ya Tanga na Halmashauri ya Jiji kwa
ushirikiano mkubwa tunaoupata katika kutoa huduma zetu za Maji safi na
uondoaji wa maji taka pamoja na utunzaji wa mazingira”Alisema

Alisema
kwa kuenzi mchango huo Tanga UWASA imeona kuna haja ya kurejesha
shukrani zake kwa jamii na serikali kwa vitendo kwa kuunga mkono juhudi
za uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule ya
msingi Saruji.

“Tanga
Uwasa ni Taasisi ya serikali inayosimamia usambazaji wa huduma ya maji
safi na uondoshaji maji taka hivyo tunapotoa vifaa hivi tunaomba
wanafunzi na wadau wote wakumbuke kwamba ubora wa huduma za maji
unatokana na utunzaji wa mazingira”Alisema

“Lakini
pia mkumbuke kulipiaji ankra kwa wakati ,ulinzi wa miuondombinu wa maji
safi na maji taka na utunzaji mazingira uendelezaji wa rasilimali watu
kama ambavyo shule inavyofanya”Alisema

Alisema
kutokana na ushirikiano uliopo na wananchi kuimarisha shughuli za usafi
wa mazingira Tanga UWASA tunajivunia jiji halina tatizo la milipuko ya
magonjwa.

Awali
akizungumza wakati wa halfa hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa aliwashukuru Tanga UWASA kwa msaada ambao wameutoa utakaosaidia
kuondosha changamoto ya uhaba wa madawati kwenye shule hiyo.

Alisema
kama Taifa chini ya Rais wamefanikiwa sana kuhamaisha watu wafahamu
umuhimu wa elimu hali ambayo imepelekea wazazi kuwa na mwamko wa
kuwapeleka watoto wao shule bila kusukumwa.

Alisema
uwepo wa mwamko wa wazazi kujua umuhimu wa elimu hayo ni mafanikio huku
akieleza kwamba Serikali peke yake haiwezi kukidhi mahitaji ambayo ni
makubwa maana yake inahitaji madarasa zaidi, walimu wengi,vifaa vingi
zaidi,na miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kumfanya mtoto asome,

“Lakini
kwa bajeti ya serikali pekee haiwezekani kutimiza mahitaji yao kazi ya
serikali ambayo imefanywa vziuri na Rais wetu ya kuelimisha na
kuhamasisha na sisi tulipo chini tunaendele kuifanya ili iweze
kufanikiwa lazima watu wenye mapenzi mwema wajitokeza kushirik katika
kutenda”Alisema 

Alisema
wanapopata watu mfano wa Tanga UWASA wanaounga mkono jitihada za Rais na
chama chake tunapata matumaini kwamba kweli Tanzania mpya sasa
inakwenda kujengeka huku akitoa wito kwa wengine kuitika wito huo.

Naye
kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Saruji Hellen Makange
alisema msaada huo wa madwati ambao umetolewa na Tanga UWASA utawasaidia
wanafunzi wa shule hiyo kuondokana na tatizo la kukaa chini ambalo
wamekuwa nalo .

“Kwa
kweli tunashukuru sana kwa msaada huo wa madawati utatusaidia kuondoa
tatizo la wanafunzi kukaa chini ambalo sio nzuri”Alisema Mwalimu hiyo.

Akizungumzia
changamoto zilizopo shuleni hapo alisema moja wapo ni kukosekana kwa
ulinzi shuleni hapo tatizo ambalo linapelekea baadhi ya shughuli kukwama
kutekelezeka kutokana na ulinzi.

“Kwa
mfano tunazo kompyuta tangu 2015 ila ni hatari kuzifungia shuleni kwani
hakuna uhakika wa usalama  lakini pia kumekuwa na udokozi na uharibifu
katika baadhi ya miundombinu ya shule”Alisema