Tcra ccc yapokea changamoto za wanafunzi wenye mahitaji maalum -patandi

 Anayezungumza ni Katibu Mtendaji kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania (TCRA CCC )Mary Shao Msuya,kulia kwake ni Mhandisi mwandamizi TCRA Jan Kaaya ,akifuatiwa na mjumbe wa Baraza
Mmoja
wa wanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi na uoni hafifu kutoka Chuo cha
Ualimu Patandi akiuliza swali kwa Baraza la Usahauri la watumiaji wa
huduma za mawasiliano Tanzania 
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo cha ualimu Patandi waliojikusanya kwaajili ya
kupatiwa elimu juu ya matumizi sahihi ya huduma ya mawasiliano na
mitandaoya kijamii kutoka TCRA CCC
 Kutoka
kushoto ni Mhandisi Mwandamizi TCRA Jan Kaaya akifuatiwa na Katibu
Matendaji kutoka TCRA CCC wakiwa Chuo cha Ualimu Patandi . Na.Vero Ignatus,Arusha
Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma Mawasiliano  Tanzania TCRA CCC limepokea
maoni pamoja na changamoto za kutoka kwa  walimu na wanafunzi wenye
mahitaji maalum katika chuo cha Ualimu cha Patandi kilichopo mkoani
Arusha na kuahidi kuyatendea kazi
Akizungumza
mara baada ya baraza hilo  kutembelea chuoni hapo na kutoa elimu ya
matumizi sahihi ya mawasiliano na mitandao  ya kijamii Katibu mtendaji
baraza hilo Mary Shao Msuya alisema kuwa ni zoezi  endelevu kwaajili ya kutoa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano nchini.
Amesema
kuwa baadhi ya changamoto nyingine wamezijibu hapohapo ila nyingine
wamezichukua na kuondoka nazo ili kuona namna gani wataweza kuboresha
huduma hizo za mawasiliano ili kila mtu aweze kuzitumia kwa manufaa na
makusudiao halali anayotaka kuyafanya
‘’Tumshauriana
nao na tumepokea maoni kutoka kwao  pamoja na changamoto mbalimbali za
huduma ya mawasiliano tumebadilishana mawazo walikuwa na maswali mengi
mengine tumeyajibu,mengine tunaenda kuyatendea kazi alisema Shao’’
Shao
aliwakumbusha watumiaji wa huduma hizo za mawasiliano kuanza kujilinda
wao wenyewe kwanza  na kuwa makini na watumiaji wengine ambao siyo
waaminifu ambao wanatumia uhalifu kama fursa kupitia mitandao hiyo
kutokuwa wepesi wa kujibu jumbe wanaz otumiwa na watu ambao hawawafahamu
Kwa umoja wao  baadhi ya wanavyuo wenye ulemavu walioshiriki na kupata elimu hiyo wameipongeza TCRA CCC Kwa
kuwatahamini na kuona umuhimu wao na kuwatembelea chuoni hapo
wamewaomba wasichoke bali pale kutakapokuwa na madadiliko yeyote katika
huduma ya mawasiliano wawatembelee na kuwaelimisha Zaidi.
Kwa upande wake Mtoa  Elimu kutoka TCRA CCC Hillary Tesha alisema
kuwa mtumiaji wa bidhaa au huduma za mawasiliano anaweza kuwasilisha
malalamiko kwa muuzaji au mtoa huduma ambapo mtoa huduma atatakiwa
kushughulikia na kujibu kwa mlalamikaji hatua zilizochukuliwa ndani ya
siku thelathini (30)
Alisema
endapo kama mtumiaji hakuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na mtoa
huduma au bidhaa mlalamikaji anaweza kupeleka malalamiko yake kwa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)