Tcra kampeni ya mnada kwa mnada chalinze katika utoaji wa elimu ya usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

Wananchi wakiwa katika foleni ya
usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada
katika Viwanja. Vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani.
Mwananchi akiweka taarifa za
usajili katika Mnada wa Chalinze wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya
TCRA ikiwa imepita kwa ajili ya kutoa Elimu ya usajili wa laini kwa
alama za vidole.
Wakazi wa Chalinze na viunga vyake
wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi
la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili
wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na
kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 15 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA
Mhandisi Lawi Odiero amesema ni fursa kwa wananchi wa Chalinze na
vyunga brake katika Uwanja wa Bwilingu wajitokeze ya kujisajili laini za
simu kwa alama za vidole na huduma nyinginezo kutokana na kuwepo kwa
mnyororo wadau wa mawasiliano.
Mhandisi Odiero amesema kuwa Mnada
kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa
wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Amesema muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe
taarifa zinazohitajika katika kujisajili laini za simu kwa alama za
vidole.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.
Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa
Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na
wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa
mawasiliano nchini.
Odiero amesema kuwa wananchi wasio
kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa
laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za
Mawasiliano hayo.
Hata hivyo Kanda ya Mashariki
itapita katika wilaya zote katika mikoa mitano ya kanda hiyo ambayo
Morogoro,Pwani Dar es Salaam, Lindi pamoja Mtwara.
Amesema kuna watu wengine
wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika
Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi
ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa
kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole
kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.
Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA
iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa
usalama kutokana na elimu tunayotoa.
Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.
“TCRA tumejidhatiti katika
kuwafikia wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za
mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema Kavishe.
Naye Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema
kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili
ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa
Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende
katika mamlaka husika kupata vitambulisho.
Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu.