Mfanyabiashara bidhaa kww njia ya mtandao Clamance Mtembela akizungumzia bei ya bando kuwa chini.
Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji
(NIT) Hamisi Mchuchuri akizungumza faida ya kushuka kwa bando kurejea
Awali kuwa kunapunguza gharama za maisha kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Mjasirimali wa Biashara ya Matunda
Walter Hiristo akizungumza kuhusiana watoa huduma kuboresha huduma ya
bando na kuipongeza TCRA kwa udhibiti .
Mkurugenzi wa TIBA Marcela Lungu
akizungumza faida ya kushuka kwa bando inavyotoa fursa katika uendeshaji
wa Ofisi katika ununuzi wa vifurushi vya Internet.
*Wadai maisha yatakuwa rahisi katika kufanya biashara mtandaoni
Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kurudisha vifurushi vya Bando wananchi wamekuwa na maoni
tofauti juu ya kuipongeza Mamlaka hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
watumiaji wa vifurushi vya Bando la Internet wamesema kuwa maisha
yalikuwa magumu kwao na huku baadhi wakishindwa kuendesha biashara kwa
kutumia mtandao.
Mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji (
NIT) mwaka wa tatu Hamisi Mchuchuri amesema kuwa bando kuwa juu lilikuwa
linawaathiri katika masomo kutokana maisha ya Chuo kuwa ya bajeti.
Amesema kuwa kuna vitabu vingine viko
mtandaoni hivyo bila kuwa fedha zaidi ya 5000 huwezi kupata lakini sasa
unapata hata sh.1000 na 2000 na kupata vifurushi vya kuweza kupakua
vitabu vyote.
Mchuchuri amesema TCRA kupitia watoa huduma za simu wameweza kuboresha huduma za bando.
Mkurugenzi wa Taasisi ya
Uhamamasishaji wa Wanawake kutumia mitandao (TIBA) Marcela Lungu amesema
kuwa kama wanaasasi walikuwa wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya bando
lakini sasa itapungua na kuweza kuwafikia wananchi kwa wakati.
Amesema wakati Ugonjwa wa Corona sehemu kubwa wanatumia mitandao kwa kununua bando kuendesha mikutano.
Kwa upannde wa Mjasirimali wa matunda
Walter Hirispo amesema miasha ya bando kuwa juu yanaathiri watu wote
hasa wenye kipato cha kuwaida kushindwa kumudu maisha hayo.
Nae Clemance Mtembela mfanyabiashara
wa Duka Mtandao amesema kuwa biashara ya bando kurejea katika hali ya
awali kumerahisha maisha kwa kuweza kuwafikia wateja wote kwa wakati na
wakawa hewani.
Amesema wakati vifurushi vilivyokuwa
juu baadhi ya watu walikuwa hawaingii mtandaoni kufanya biashara na hata
wakiingia hawawezi kupakua huduma ndani ya mtandao