Tcra yatoa mafunzo utekelelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi kwa watendaji mamlaka za serikali za mitaa singida

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi 
akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na
postikodi kwa watendaji  mamlaka za serikali za mitaa Manispaa za Mkoa
wa Singida leo ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA). Kulia ni  
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio
Manyanda na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
 Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida, Michael Moses,akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi, akizungumza.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Katibu
Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida, Michael
Moses, akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.Kulia ni Katibu Tawala
Msaidizi Afya (RMO), Dkt. Victorina Ludovick.

 Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda, akitoa taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi.

 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea. 
 Afisa Masoko wa TCRA, Abdulrahaman Millas Issa, akitoa mada kuhusu anwani za makazi na postikodi.
 Afisa Mwandamizi wa TCRA, Dorice  Mhimbira, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakielekea Mtaa wa Ipembe mjini Singida kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.
 Afisa
Masoko wa TCRA, Abdulrahaman Millas Issa, akiwaelekeza washiriki wa
mafunzo hayo namna ya kuandika namba kwenye nyumba katika mtaa wa
Ipembe. 
Washiriki
wa mafunzo hayo wakielekea eneo la Kilambida lililopo Kata ya Kindai
mjini Singida, ambalo nyumba zake zimejengwa bila ya kufuata mipango
miji  kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
MPANGO wa kuweka mabango ya anwani za makazi na postikodi usifanywe kisiasa bali ufuate taratibu na sheria zilizowekwa.
 
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi
wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na
postikodi kwa watendaji  mamlaka za serikali za mitaa Manispaa za Mkoa
wa Singida leo ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) 
 

Suala ili naomba lisifanywe kisiasa lifuate sheria na taratibu zilizopo
kwani katika maeneo mengine lilichelewa kufanyika kutokana na wanasiasa
kutaka majina yao yawekwe kwenye vibao vya mitaa” alisema Nchimbi.
 
Alisema
mpango huu wa kitaifa ni muhimu sana kwani unasaidia wakati wa matukio
ya dharura kama moto na kuwafuata wagonjwa katika maeneo yao
yanayojulikana tofauti na ilivyo hivi sasa.
 
Nchimbi
alitaja faida nyingine kuwa utaweka vizuri mipango miji katika maeneo
wanayoishi wananchi na utapunguza migogoro ya ardhi na utambuzi wa watu
wanapoishi na kupata huduma 
za kijamii kwa urahisi.
 
 Nchimbi
alitumia nafasi hiyo kuwaomba wataalamu wa mkoa wa Singida ambao
wamepata mafunzo hayo kwenda kufanya kazi hiyo kwa bidii na weledi huku
wakiweka maslahi ya Taifa mbele.
 
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda alisema TCRA
imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika mradi huo kama ilivyoelekezwa
katika sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 ambayo inalenga kuboresha
maisha ya watanzania kwa kupambana na umaskini.
 
Alisema
mpango huo ulianza katika jiji la Arusha ambapo baadhi ya kata
ziliwekewa miundombinu ya anwani kama sehemu ya mfano (pilot) na baada
ya hapo uliendelea katika jiji la Dodoma ambapo ushahidi wa miundombinu
unaonekana.