Tfs watoa msaada wa viti, meza na madawati wilayani muheza

 

Mkuu
wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa
madawati,viti na meza  kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti
Longuza Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na
Ofisi za Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na
Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS)

Mkuu
wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa
madawati,viti na meza  kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti
Longuza Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na
Ofisi za Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na
Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS)

MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo kulia akimkabidhi msaada huo Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza mara baada ya kuvipokea kulia ni Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema
Mwasalanga

MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano iliyofanyika wilayani humo kulia  ni Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema
Mwasalanga

Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema
Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano

Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema
Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano

Meneja
Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano

MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo katika akiwa na Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema
Mwasalanga
kulia akifuatiwa na  Meneja
Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama

Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo

Sehemu ya madawati yaliyotolewa

NA OSCAR ASSENGA, MUHEZA

WAKALA wa
Huduma za Misitu TFS shamba la Lunguza lililopo wilayani Muheza mkoani
Tanga wametoa msaada wa madawati, viti na Meza vyenye thamani ya sh
mil17. 4

Msaada huo
ambao ni kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari Tatu ambazo ni pamoja
na Ofisi za watendaji kata mbili zilizopo wilayani Muheza utasaidia
kuondosha changamoto zilizokuwepo awali.

Akikabidhi
msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo, Mhifadhi wa
shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga alisema kuwa msaada huo ni
kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa huduma.

“Tumetoa viti na Meza 17 kwa ajili ya Ofisi za watendaji na madawati 60 kwa shule za msingi na Sekondari” alisema Mwasalanga.

Awali
akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo aliishuku TFS kwa
namna walivyothamini elimu ya Watoto wa kitanzania na hivyo kwa msaada
huo wataweza kuboresha utoaji wa elimu.

Mkuu huyo wa
wilaya alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa
kuilinda misitu kuhakikisha hakuna uharibu unaofanyika.

“Niwaombe
wananchi huu msitu unatunufaisha hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha
tunaulinda ili uweze kutusaidia katika kukuza kipato chetu na uchumi”
alisema DC Bulembo

Naye kwa
upande wake Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha
Chasama alisema wametoa madawati 60 ambapo kati ya hiyo madawati 30
wametoa kwenye shule ya Msingi Kwemdimu, madawati 30 shule ya Sekondari
Potwe na madawati 30 wametoa shule ya Sekondari Amani.

Alisema pia
wametoa viti na meza 17 ambavyo wametoa ambapo thamani hizo ni
sh.milioni 17.1 wao kama wahifadhi wanasema wahifadhi wa baadae ni
watoto wadogo ambao wamewatolea thamani hizo.

“Misaada hiyo
wanayoitoa kwa shule hizo na ofisi za watendaji tunaomba thamani hizo
zitunzwe pamoja na walimu waangalia watoto namna wanavyocheza kwa sababu
wakati mwengine wanaweza wakawa wanabonda madawati  ili nao kama wakala
wa huduma za misitu Tanzania (TFS) waweze kupata nguvu ya kuendelea
kutunzwa zaidi”Alisema