The sunrise nursery and day care centre mahafali ya 3, kila mwaka watoto 5 kusoma bure, mwenyekiti habiba jumanne ahimiza wazazi na walezi, smaujata shinyanga yatoa elimu

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wazazi na walezi wanaoishi na watoto chini
ya umri wa kuanza darasa la kwanza katika Manispaa ya Shinyanga wameshauriwa kuwapeleka
watoto wao kwenye vituo vya elimu ya malezi ya awali kwa watoto (Day Care) ili waweze
kuwa na msingi bora wa elimu.

Ushauri huo umetolewa na Mgeni rasmi
katika mahafali ya tatu kwenye kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery
and Day Care Centre, Mwenyekiti wa mtaa wa Kitangili Bi. Habiba Jumanne ambapo
amesema ni muhimu watoto kupata elimu ya malezi ya awali kabla ya kuanza darasa
la kwanza.

Mwenyekiti huyo Bi. Habiba Jumanne ametumia
nafasi hiyo kuwaomba wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto wao
wanapata elimu ya malezi ya awali ili kuwatengenezea misingi bora ya elimu
wawapo shule ya msingi.

Akizungumza mkurugenzi wa  kituo cha malezi ya watoto The Sunrise
Nursery and Day Care Centre kilichopo mtaa na kata ya kitangili Manispaa ya
Shinyanga Bwana Ndaki Mathias amesema kila Mwaka kuna utaratibu wa watoto
watano kupata elimu ya malezi ya awali bure 
hasa wanaoishi katika familia zenye kipato cha chini.

Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria
mahafali hayo wamewapongeza na kuwashukuru walimu wa kituo hicho kwa
kuwaimarisha watoto wao huku wakisema ni muhimu watoto kupata elimu ya malezi
ya awali kabla ya kuanza darasa la kwanza.

Jumla ya watoto 27 wamehitimu Mwaka huu
2023 katika kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre
kilichopo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya
Kitangili Mhe. Mariam Nyangaka awapongeza wazazi kwa kuwapa kipaumbele watoto
katika suala la elimu huku akiwaomba wazazi na walezi kuwapelekea watoto
shuleni ili kupata haki yao ya elimu.

Aidha Mhe. Nyangaka ametumia nafasi hiyo
kuwataka wananchi wa kata ya Kitangili kuendelea kuchukua tahadhari ya Mvua
nyingi zinazotajwa kuwa ni Mvua za El nino ambapo Mkoa wa Shinyanga ni moja ya
Mikoa inayotajwa kuathirika na Mvua hizo.

Katika mahafali hayo viongozi wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga akiwemo Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel
Kapaya pamoja na Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana
Solomon Nalinga Najulwa (Cheupe) wametoa elimu ya ukatili kwa watoto, wazazi,
walezi na wananchi wote waliohudhuria sherehe hiyo.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
wamewakumbusha wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mazuri huku
wakiwasisitiza kuimarisha ulizi na usalama kwa watoto wawapo nyumbani lakini
pia nje ya familia yao na kwamba hali hiyo itachangia kuwaepusha na ukatili.

Viongozi hao wameitaka jamii kuacha
vitendo vya ukatili huku wakiwasihi kutoa taarifa za ukatili sehemu huzika au
kupiga namba ya bure 116 kutoa taarifa za ukatili ili hatua za kisheria ziweze
kuchukua kwa wahalifu.

Wametumia nafasi hiyo kuviekeleza vituo
vya kulea watoto kuweka mabango yenye ujumbe wa kupinga ukatili katika
mazingira ya shuleni au vituoni ili watoto waweze kuwa na tahadhari katika
kuepukana na ukatili.

Viongozi wa kampeni ya kupinga ukatili
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wameendelea kutoa elimu ya ukatili sehemu mbalimbali
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili.

 

Mgeni rasmi katika mahafali ya tatu kwenye
kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre, Mwenyekiti
wa mtaa wa Kitangili Bi. Habiba Jumanne akiwasili ukumbini.


Wazazi, walezi na wananchi mbalimbali
waliohudhuria mahafali ya tatu Mwaka huu 2023. katika kituo cha malezi ya
watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre kilichopo Manispaa ya Shinyanga.