Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari akizindua kampeni
iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwa ajili ya wateja wanao tumia Tigo
Pesa. kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta.
iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwa ajili ya wateja wanao tumia Tigo
Pesa. kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta.
Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kampeni iitwayo
kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa Mkuu
wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kampeni iitwayo
kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa Mkuu
wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari
-
Zawadi zenye thamani ya zaidi ya 500m/- kutolewa kwa washindi
Dar es Salaam, 25 Novemba, 2019. Kampuni ya Tigo, kupitia kitengo cha Tigo Pesa imezindua kampeni ijulikanayo kama ‘Kishindo cha Funga Mwaka’ kwa ajili ya kutoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya 500m/- kwa wateja wa Tigo wanaoweka na kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa.
Wateja wa Tigo wanatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa ili kuweza kushiriki kwenye kampeni hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya msimu huu wa kufunga mwaka ambapo washindi wa zawadi watafunga mwaka kwa kishindo
Kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja itashuhudia washindi watatu wakiibuka na fedha taslimu ikiwamo 20m/- kwa mshindi wa kwanza, 15m/- kwa mshindi wa pili na 10/- kwa mshindi wa tatu. Pia, kila wiki kutakua na washindi nane watakaopata 5m/- kila mmoja. Pamoja na washindi wa wiki na wa mwezi, kutakua na washindi nane kila siku ambao wataibuka na 1m/- kila mmoja.
“Wateja wanatakiwa kuweka pesa kwa Wakala au kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa kutoka benki, mitandao mingine au vyanzo vingine mbalimbali na moja kwa moja watakuwa kwenye nafasi ya kushinda. Hakuna gharama yoyote ya kuweka au kupokea pesa kwa Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa – Tigo Pesa, James Sumari, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Kwenye kampeni hii hakuna masharti ya kushiriki kwa mteja wa Tigo Pesa isipokuwa; kadiri unavyoweka pesa nyingi ndivyo unajiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
“Tunategemea kupata washindi wapatao 331 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja wa kampeni yetu na lengo kubwa ni kuonesha na kurudisha shukrani kwa wateja wetu kwa kuwa pamoja na Tigo Pesa kwa kipindi cha mwaka mzima,” alisema Sumari.
Huduma ya Tigo Pesa imeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu, na kuongeza huduma na bidhaa bora zaidi ikiwamo kutoa mikopo, huduma za bima na huduma kwa makampuni na taasisi zinazowezesha kulipa na kukusanya pesa kwa ufanisi jambo linaloifanya Tigo Pesa kuwa huduma kamili ya kifedha ikiwa na mawakala zaidi ya 150,000 nchi nzima.