Tpdc -kuunganisha gesi asilia katika nyumba 400 mwaka huu


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
 
SHIRIKA la Maendeleo
ya Petrol Tanzania (TPDC) linatarajia kuunganisha nyumba 400
kupitia mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ,ambapo kati ya
nyumba hizo nyumba125 zitakuwa mkoa wa Mtwara na nyingine  mkoa wa Dar
es Salaam.
 
Aidha mpaka sasa
viwanda 45 vinafanya uzalishaji kwa kutumia gesi inayosambazwa na TPDC
na miongoni mwa viwanda hivyo ni DANGOTE kilichopo mkoani Mtwara na
Goodwill kilichopo Mkiu wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani.
 
Mtaalamu mwandamizi
wa masuala ya Petroli(Geologist)kutoka TPDC Simon Zablon,alisema hayo
katika  maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea kufanyika kwenye
viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani Mjini Kibaha.
 
Alisema, nyumba hizo zinatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu.
Zabron alisema,katika upande wa  viwanda ambavyo vitanufaika na mradi huo ni kiwanda cha Lodhia, NAF na Cokacola .
 
“TPDC tupo tayari
kutoa huduma ya gesi  kwa urahisi kwenye viwanda vyote vilivyopo katika
Mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na ambavyo miundombinu ya bomba la gesi
imepita”
Katika hatua
nyingine, alifafanua magari yanayotumia gesi hadi sasa yamefikia 200,
na  kwamba magari yanayounganishwa na huduma hiyo ni yale yaliyokuwa
kwenye mfumo wa kutumia petroli.
 
Alisema, awali mradi
wa kuunganisha gesi kwenye magari ulianza miaka saba iliyopita lakini
ulikuwa unasuasua kutokana  muamko kwenye vituo vya mafuta kuwa mdogo .
 
Zabron alielezea pia
kumetokana na kituo kimoja kilichokuwa Ubungo jijini Dar es salam pekee
kutoa huduma hiyo tofauti na hali ilivyo sasa.