Tucta lataka haki kwa wafanyakazi shinyanga, rc mndeme atoa maagizo kwa waajili.

Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imewataka
waajili wa sekta binafsi kufuata kanuni na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa stahiki zao kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga baada ya kupokea changamoto kutoka shirikisho la wafanyakazi TUCTA
Mkoa wa Shinyanga kwenye maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Mei Mosi ambayo kimkoa yamefanyika
katika Wilaya ya Kishapu.

Katika risala iliyosomwa na mratibu wa
TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Ramadhan Pangara ametaja baadhi ya changamo
zinazowakabili wafanyakazi Mkoani Shinyanga huku akiiomba serikali
kushughulikia.

“Changamoto
zinazotukabili sisi wafanyakazi wa Mkoa wa Shinyanga katika Utumishi wa Umma na
pia wafanyakazi wa Sekta Binafsi kama ifuatavyo baadhi ya waajiri wa Sekta
Binafsi kutozingatia sheria, Kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa na serikali”

”Jambo hili imesababisa changamoto zifuatazo
kutotolewa kwa Mikataba ya ajira na Waajiri, kuwazuia wafanyakazi kutojiunga
vyama au kuachisha kazi Wale wanaojiunga na vyama vya wafanyakazi jambo ambalo
ni kinyume na sheria ya Ajira na Mahusiano kazini sura ra 366 rekebisho la
2019, baadhi ya Waajiri hawawachangie watumishi wao au hawapeleki michango kwa
wakati kwenye mifunko ya hifadhi ya jamii, baadhi waajiri hawatoi hati za
malipo ya Mishahara kwa Wafanyakazi, waajiri binafsi kutozingatia waraka wa
Mishahara wa mwaka 2022, kwa kima cha chini, ambao utekelezaji wake umeanza Januari
2023”.amesema mratibu Pangara

“Tunaiomba
Serikali isimamie kwa ukaribu sana taratibu za ajira katika sekta binafsi kama
ilivyo katika sekta ya Umma ucheleweshwaji wa Mafao ya Kustaafu kwa wafanyakazi
kutoka Katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamil imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa
wastaafu wengi ambao warnelitumikia Taifa hili kwa uadilifu kwa muda mrefu.
Baadhi Ya wastaafu warnejikuta wakipoteza maisha hata kabla hawajalipwa mafao
yao ya kustaafu. Tunaomba wastaafu wetu walipwe mafao yao mara tu baada ya
kumaliza likizo yao ya mwisho ya kustaafu”

“Madai
mbalimbali ya Uhamisho, Mapunjo ya Mishahara Malipo Ya nauli za likizo,
Matibabu na gharama za masomo imekuwa kero kubwa hasa kwa watumishi katika
sekta ya Umma japo malipo haya yanafanyika lakini si kwa wakati na kwa kiwango
ambacho kingewamotisha wafanyakazi hawa Tunaomba sana serikali ya awamu ya Sita
ichukue hatua madhubutj kuondoa kabjsa kero hizi ikiwa ni pamoja na kulipa
nauli kabla mtumishi hajaenda likizo ya malipo.”.amesema mratibu TUCTA

“Waajiri
wa Sekta za Umma na binafsi kutozingatia na kudhoofisha haki za kioganaizesheni
za wafanyakazi Jambo hili limesababisha mambo yafuatayo, kutozingatiwa kwa
Mikataba ya Utambuzi na Majadiliano ya pamoja, Kutofuatwa kwa masharti
yanayounda mabaraza ya Wafanyakazi na hata kwa baadhi ya waajiri sekta za Umma
hasa Halmashauri kutofanya Mabaraza ya Tathmini baadhi ya waajiri kutotoa
wafanyakazi hodari ama kutenga bajeti ndogo kwa ajili ya kuwamotisha
wafanyakazi”

“Viongozi
wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Trade Union Congress of
Tanzania) TUCTA kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga tunapenda
kutumia fursa hii kukushukuru kwa moyo wa dhati, kupokea na kukubali mwaliko
wetu na kushiriki nasi katika siku hii ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambayo
Kimkoa inafanyika hapa Wilaya ya Kishapu tunasema asante sana”

“Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Shinyanga linawakilishwa na jumla ya Vyama
shiriki vipatavyo kumi ambavyo ni COTWU (T), CWT, CHODAWU, TAMICO, TALGWU,
TEWUTA, TUGHE, TUICO, TPAWU na RAAWU”

“Tunaungana
na Watanzania wote kuipongeza kwa dhati serikali ya awamu ya Sita kwa juhudi
nyingi zinazofanywa katika Taifa letu kama kuboresha mahusiano ya kitaifa na
kimataifa, kuweka mazingira mwafaka kwa wawekezaji, kuitangaza Nchi kimataifa,
kuongeza Ajira katika utumishi wa Umma, na kuendelea kusimamia vyema
utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati katika Nchi yetu”

“Katika
Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu 2023 yenye Kauli Mbiu Isemayo “Mishahara
Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa maendeleo ya Wafanyakazi” Wakati ni
Sasa! Kauli mbiu hii imetokana na hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kutokana
na uwepo wa Mishahara midogo na Maslahi duni yasiyokidhi hali na gharama za
maisha kwa sasa”

 “Hivyo tunaiomba Serikali na wamiliki wa
Makampuni binafsi pamoja na Viwanda wazingatie Uboreshaji wa Mishahara na
Maslahj kwa wafanyakazi wa Nchi ili iendane na gharama halisi za
Maisha”.amesema mratibu Pangara

“Aidha,
tunaendelea kusisitiza waajiri wote watoe Mikataba ya ajira inayokidhi viwango
Wa kisheria, kufanya Majadiliano ya pamoja (Mikataba ya Hali Bora, Mabaraza ya
Wafanyakazi) ili kutatua changamoto zilizopo na kupunguza migogoro sehemu za
kazi na hatimaye kupatikane Tija na Ufanisi katika sehemu za kazi”

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa
Shinyanga Bwana Mathias Balele  ameipongeza
serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo ameiomba serikali kufanya kikao cha
pamoja ili kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ile ya Kikokotoo.

“Ni
kweli watumishi wetu wamekuwa wakipata shida sana kwa sababu sheria haieleweki
kwa wanachama wetu kwa mfano tuliambiwa kwenye kikokotoo kulingana na kanuni
mafao ya mwisho wa mwezi yataongezeka lakini tunayo mifano kuna wafanyakazi
wetu waliostaafu Miaka miwili kwa daraja lilelile kwahiyo tunaiomba serikali
ikae meza moja na shirikisho la vyama vya wafanyakazi wakae meza moja na
mawaziri wakaangalie upya kanuni hizi zipate kuwabeba watumishi wetu wa
Tanzania”.amesema Mwenyekiti Balele

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka waajili katika sekta
binafsi kuzingatia sheria huku akimwagiza katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga
kufuatilia ili kubaini taasisi za umma zinazokiuka sheria za kazi na maelekeozo
ya serikali.

“Madai
ya watumishi wa umma na sekta binafsi yakiwemo ya likizo, uhamisho na
malimbikizo ya mshahara niwatake waajili wa sekta binafsi kuhakikisha
wanawalipa madai watumishi kwa wakati na kwa upande wa serikali watumishi wa
umma maelekezo yamekwisha tolewa watumishi wa umma wasihamishwe bila kulipwa
stahiki zao”

“Niwatake
waajili kuhakikisha kuwa mnatenga fedha kwenye bajeti zetu kwa ajili ya likizo
na stahiki zote za watumishi kuhusu baraza la wafanya kazi katika sekta za umma
kutofanya vikao vya mabaraza ya wafanyakazi na kutolipa stahiki zao kwa mujibu
wa sheria ninakuagiza katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga ufuatilie hili na
uniletee orodha ya taasisi za umma zinazokiuka walaka wa serikali’”.amesema RC
Mndeme

RC Mndeme ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na serikali katika
kutokomeza ukatili unaoendelea huku akisisitiza jamii hasa wazazi na walezi
kusimamia maadili mema kwa watoto ili kuwaepusha na mmomonyoko wa maadili
ikiwemo kujiingiza kwenye makundi mabaya na wengine kwenda kinyume na mila na
desturi za Nchi.

Pia mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya
usalama kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu
wenye nia mbaya katika Mkoa huo.

Amewaangiza viongozi wenye mamlaka katika
serikali za mitaa Mkoa wa Shinyanga kuweka utaratibu wa kaya kutopokea wageni
pasipo kutolewa taarifa kutoka kwenye uongozi wa vitongoji na vijiji ili
kuimarisha usalama na kwamba hali hiyo itasaidia kuendelea amani ya Nchi.

Akitoa salam kwa niamba ya wakuu wa Wilaya
za Mkoa wa Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bwana Joseph Mkude ametumia
nafasi hiyo kuwasihi wafanyakazi kutimiza wajibu wao kila mmoja katika nafasi
yake bila kujali changamoto zinazowakabili huku akiwasisitiza kuepuka migogoro
hasa sehemu za kazi ambapo amewahimiza kufanyakazi kwa upendo, umoja,
kuheshimiana pamoja na kushirikiana ili kuendeleza tunu ya Taifa.

Sherehe za maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi Duniani Mei mosi katika Mkoa wa Shinyanga imefanyika katika uwanja
Mwadui Complex Wilaya ya Kishapu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa na
serikali na taasisi binafsi  ambapo mgeni
rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa  Shinyanga
Bi. Christina Mndeme.

Katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mwaka huu
2023 kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro kauli Mbiu inasema “MISHAHARA
BORA NA AJIRA ZA STAHA NI NGUZO KWA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI” Wakati ni
Sasa!

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi mei mosi katika uwanja wa Mwadui Complex uliopo
Wilaya ya Kishapu.

Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana
Mathias Balele akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi  mei mosi  katika uwanja wa Mwadui
Complex uliopo Wilaya ya Kishapu.

Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana
Ramadhan Pangara  akisoma risala kwenye
maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi mei mosi  yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kishapu.

Akitoa salam kwa niamba ya wakuu wa Wilaya
za Mkoa wa Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bwana Joseph Mkude leo katika
maadhimisho ya mei mosi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga upande wa
kulia Mhe. Johari Mussa Samizi, mkuu wa Wilaya ya Kahama katikati Mhe. Mboni Mhita
pamoja na Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga upande wa kushoto Mhe. Elias Ramadhan
Masumbuko wakiwa katika maadhimisho ya Mei mosi  yaliyofanyika katika uwanja
wa Mwadui Complex Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana
Ramadhan Pangara akitambulisha wageni waliohudhuria maadhimisho hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko upande
wa kushoto wakiwa katika maadhimisho Mei mosi katika uwanja wa Mwadui Complex Wilayani
Kishapu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya Mei mosi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mathias Balele upande wa kulia wakiwa katika maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi mkoani humo.

Katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria sherehe hiyo ya Mei mosi Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita .

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi.

Viongozi mbalimbali wa serikali akiwepo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura wakiwa katika sherehe za siku ya wafanyakazi Mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mathias Balele akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi (Mei mosi) 2023 katika uwanja wa Mwadui Complex Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa katika maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi.Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mathias Balele upande wa kushoto akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kutoa hotuba yake katika maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi Mkoani Shinyanga.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi (Mei mosi) ambapo kimkoa imefanyika katika uwanja wa Mwadui Complex uliopo Wilaya ya Kishapu.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi (Mei mosi) ambapo kimkoa imefanyika katika uwanja wa Mwadui Complex uliopo Wilaya ya Kishapu.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti na zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti na zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti na zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Tazama picha za mabango yenye ujumbe mbalimbali juu ya maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi Duniani ambapo Mkoawa Shinyanga  imefanyika katika Wilaya ya Kishapu.