Tundu lissu amepona lakini anahofia usalama wake kurudi tanzania

Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeelezwa kuwa aliyekuwa Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameshapona ila anashindwa kurudi
nchini kwa kile alichokidai ni kuhofia usalama wake.


Hayo
yameelezwa leo Novemba 21,2019 na Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Ahmed,
alipokuwa akiieleza mahakama hiyo juu ya afya ya Mwanasheria huyo wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ahmed
ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,
wakati wa kesi ya uchochezi inayomkabili mshtakiwa huyo na wenzake
watatu ilipoitwa.