Ubora wa viwanda vya nyama nchini wachochea kasi ya usafirishaji wa nyama nje ya nchi

 

   


Kasi ya kusafirisha nyama
kwenda nje ya nchi imeongezeka kutokana na kuwepo kwa ubora wa Viwanda
vya nyama ikiwa ni uwekezaji mkubwa uliopo jambo linalosababisha kuwepo
kwa nyama bora na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kukidhi
soko la ndani na nje ya nchi.


Hayo yamesemwa na Kaimu
Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Bwana Imani Sichalwe akiwa kwenye
ziara ya kukagua mazingira ya usafirishaji wa nyama kutoka Tanzania
kwenda nchi za nje aliyoifanya tarehe 16.01.2021 katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Jijini Dar.


Uwepo wa viwanda hivi vya
nyama vya kisasa hapa Nchini ndio vinafanya tuwe na ithibati ya kupeleka
nyama nje ya nchi ambapo kiwanda Cha Tanchoice kilichopo Kijiji cha
soga wilayani Kibaha Mkoani Pwani chenye uwezo wa kuchinja mbuzi 4500
kwa siku na ng’ombe 1000 kwa siku moja ambapo kwa Tarehe 16.01.2021
kimepeleka mbuzi 2000 waliochinjwa Sawa na kilo 20,000 au tani 20 kwenda
Oman na Kuwait.


“Kwa Sasa kwa wiki kiwanda cha
nyama cha Tanchoice kilichopo Kibaha Mkoani Pwani husafirishwa mbuzi
waliochinjwa 6000 sawa na kilo 60,000 sawa na tani 60 kwenda Omani,Qatar
na Kuwait na kwa wiki ijayo kiwanda kitaanza kupeleka nyama katika soko
jipya la Hongkong. Kwa upande wa kiwanda Cha Nyama Cha Eliya Foods
Overseas Limited kimeanza kupeleka nyama kwenda Oman Mbuzi 1874 sawa na
tani 14.6” amesema Sichalwe.


Katika ziara hiyo ya kukagua
mazingira ya usafirishaji wa nyama kwenda nje ya nchi Kaimu msajili Bodi
ya Tanzania amesema ameridhika na namna shughuli nzima ya utaratibu
unaofanywa kuanzia kushusha nyama kwenye gari,kuingiza kwenye vyumba
maalumu vya kuhifadhia nakupooza pamoja na namna ya upakiaji wa nyama
hizo kwenye ndege