Uchumi wa marekani umeshuka kwa asilimia 32.9 kutokana na janga la corona, ikiwa ni pigo kwa rais donald trump kuelekea uchaguzi mkuu mwezi novemba.

 Mwandishi wetu na Mashirika ya Kimataifa

Kushuka kwa uchumi nchini Marekani kumeshuhudiwa kati ya
mwezi Aprili na Juni, kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya uchumi, katika
kipindi ambacho nchi hiyo imekuwa ikishuhudiwa idadi kubwa ya maambukizi ya
virusi vya Corona.

 

Mwezi Aprili pekee, zaidi ya ajira
Milioni 20 zilipotea nchini humo, baada ya biashara nyingi kufungwa na watu kusalia
nyumbani kutokana na janga la Corona ikiwa ni kutekeleza agizo la mamlaka wa
kiserikali nchini humo.

 

Wiki iliyopita pekee, watu Milioni
Moja na Laki nne waliripoti kupoteza ajira katika taifa hilo lenye uchumi
mkubwa duniani, wakati huu wachambuzi wakibashiri kuwa hali huenda ikawa mbaya
zaidi katika siku zijazo kabla ya uchumi kuanza tena kuimarika taratibu.

 

Wanasaisa wa chama cha Republican
na Democratic, wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu namna ya kuimarisha tena
uchumi wa taifa hilo kutokana na janga la Corona wakati huu taifa hilo
likielelea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Nevemba.

 

Wakati hali hii ikionekana kuathiri maelfu ya wananchi
katika nchi ya Marekani, nchi za Afrika hali ni tete baada ya ugonjwa huo
unaozuia madhara katika fumo wa hali ya hewa kuendelea kuua watu wengi Zaidi.

 

Hali hiyo imekuwa tishio kubwa la kuibuka kwa tatizo la
njaa kutokana na nchi nyingi wananchi wake kushindwa kuzalisha baada ya
kutakiwa kukaa ndani na nchi zao ikiwa ni njia ambazo wamekuwa kuzifuata ili
kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

 

Nchini Tanzania wananchi wameendelea kufanyakazi za
uzalishaji kama kawaida baada ya Serikali yake kukataa kuzuia shughuli za
uchumi kutoendelea kwa kuwafungia ndani wananchi wake jambo ambalo limeendelea
kupongezwa na wananchi mbalimbali.