Uhamasishaji wananchi kwenye miradi ya uipanuzi iia( densification iia) yaendelea mkoani tabora

 

 Timu ya wataalamu wa Tanesco kitengo
cha masoko makao makuu ikishirikiana na ofisa huduma kwa wateja mkoa wa
Tabora umeendelea na zoezi la uhamasishaji wa wananchi kwenye miradi
inayotekelezwa na wakala wa umeme vijijini REA kupitia mkandarasi wa
umeme kampuni ya Sengerema Electrica group (SEGL) ili kuandaa wananchi
kuanza maandalizi ya wiring kwenye nyumba zao mkoani Tabora.

Pamoja na kuanza maaandalizi ya
utandazaji wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba pia wananchi hao
wamepata fursa ya kujifunza maswala mbali mbali yanayohusu taratibu za
kufuata ili kujiunganishia huduma ya umeme, Gharama ya kuunganisha
umeme, wigo wa mradi kwenye maeneo yao, matumizi ya UMETA na umuhimu wa
kutunza miundombinu ya shirika ikiwemo tahadhari ya kuchoma moto hovyo
hasa wakati wa kiangazi.

Wanchi pia wamepata fursa ya kuuliza
na kupata elimu mbalimbali zinazohusiana na huduma za ki-Tanesco kama
vile makundi ya matumizi ya wateja, adha iliyojitkeza ya manunuzi ya
LUKU kwa siku za karibuni, na hali ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo
yao.

Wananchi wa maeneo mengi bado
wameendelea kulalamikia wigo mdogo wa mtandao wa miundombinu ya umeme
kwenye maeneo huku wakisisitiza kuwa hata miradi ya upanuzi bado haiwezi
kutatua mahitaji yao kwani maeneo mengi bado yameachwa.

Zoezi la uhamasishji unaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa
Tabora(Sikonge, Urambo, Kaliua, Uyui, Nzega na Igung) isipokuwa Tabora
manispaa ambayo haijanufaika na mradi wa upanuzi IIA(Densification IIA).