Ujenzi wa daraja lililokatika barabara kuu ya dodoma-morogoro waanza kwa kasi…..waziri wa ujenzi, naibu wake, mkuu wa mkoa wako eneo la tukio

Waziri
wa ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe, naibu waziri, Elias Kwandikwa, mkuu
wa mkoa wa Morogoro na viongozi wa wizara wamewasili katika eneo la
Kiyegeya lilipokatika daraja kwa kazi ya kurudisha mawasiliano ya
barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.

Kazi
ya matengenezo ya daraja hilo imeanza kwa kuweka vifusi na mawe huku
madaraja mawili ya chuma yakiwa yanaunganishwa ili kufungwa kwenye eneo
lilipokatika.

Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema Serikali imejipanga
kuhakikisha inafanya matengenezo kwa haraka ili mawasiliano yaweze
kuendelea kwani barabara hiyo inategemewa kiuchumi si kwa mikoa ya Kanda
ya Kati na ziwa pekee bali hata nchi jirani za maziwa zikiwemo Uganda,
Burundi, Congo.


Amesema muda si mrefu madaraja ya chuma yatafungwa eneo hilo ili
kupitisha maji na baadaye waanze kuweka mawe ya kutosha ili mawasiliano
yarejee. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *