Ujenzi wa madaraja mawili kata za kitangili, ibinzamata wafikia asilimia 90 ya utekelezaji, wananchi waipongeza serikali.

Na Stela Shija Shinyanga

Ujenzi
wa mradi wa madaraja mawili yanayounganisha Kata za Kitangili na Ibinzamata zilizopo
katika Manispaa ya Shinyanga umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake.

Hayo
yamebainishwa na Injinia anayesimamia ujenzi huo kutoka Wakala wa Barabara za
Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, ambapo
amesema ujenzi huo ulianza Mwezi Januari, 2023 na unatarajiwa kukamilika
ifikapo Juni 24, 2023.

Mhandisi
Yambi amesema mpaka kukamilika kwa mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi
milioni 199
fedha ambazo zinatokana na mfuko wa jimbo zinazolenga kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkandarasi yupo katika hatua nzuri ambapo
mpaka sasa ameshafikia asilimia 90 za utekelezaji, daraja la kwanza
tumeshakamilisha ujenzi na tumesharuhusu wananchi kupita kwa muda wakati
tunaendelea na ukamilishaji wa kazi zinazohusiana na barabara, maana mradi huu
umegawanyika katika sehemu kuu mbili”
amesema Mhandisi Yambi.

Tutachonga barabara na kuweka molamu karibu
na daraja, ambapo kwa ujumla utekelezaji unaendelea vizuri, na kama nilivyosema
hapo awali mradi huu unatekelezwa kwa fedha za miradi ya maendeleo ya jimbo. Na
kwamba bajeti yake ilitengwa shilingi milioni 200 lakini kulingana na mkataba
mpaka tunapotegemea kukamilisha mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi milioni
199, 968, 250/=
” ameongeza Mhandisi Yambi.

Aidha,
Mhandisi Yambi amesema asilimia 10 ilizobaki ni pamoja na kumwaga molamu karibu
na eneo la daraja, kuweka alama za daraja, na kupaka rangi kwenye madaraja
yaliyojengwa.

Ujenzi huu umetekelezwa kwa asilimia 90,
hiyo asilimia 10 ilizobaki ni kazi ndogo ndogo za umaliziaji kuna kazi ya
kuweka molamu karibu na eneo la madaraja, kuweka alama za madaraja ambapo
tutaweka alama nne katika madaraja haya mawili, tutaweka alama inayohusiana na
uzito wa magari mwisho kabisa tutapaka rangi kwenye madaraja na kazi itakuwa
imekamilika kwa asilimia 100
” amesema Mhandisi Yambi

Kwa
upande wao baadhi ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na kuipongeza serikali kwa
uboreshaji wa miundombinu hiyo, wamesema madaraja hayo yatarahisisha
wamasiliano kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ikilinganishwa na hapo
awali ambapo walikuwa wakipata usumbufu hasa wakati wa masika.