Ukarabati wa mto lukosi ruaha mbuyuni wakamilika

 Mhandisi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Daniel Manase
akizungumzia kuhusu kazi ya kurejesha Mto Lukosi katika njia yake asili,
Ruaha Mbuyuni Mkoani Iringa.
 

Mtambo aina ya Excavator ukifanya kazi ya kuiinua tuta kwa kupanga mawe
katika mto Lukosi, ili kuurejesha katika njia yake ya asili.


Picha ni Banio linalotumika kupitisha maji kutoka katika chanzo na kupeleka katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Ruaha Mbuyuni

Picha inaonesha Muonekano wa Tuta, likiendelea kufanyiwa kazi katika mto Lukosi, Ruaha Mbuyuni

 

Na Mwandishi  Wetu,Ruaha Mbuyuni–Iringa

Ukarabati
wa kingo za Mto Lukosi uliyopo katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa,
unayopeleka Maji yake katika mto Ruaha mkuu na kutumika katika skimu ya
kilimo cha Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni, umekamilika baada yakusombwa na
mafuriko makubwa yalitokea mwaka jana, yaliyosababishwa na mvua kubwa
zilizonyesha katika ukanda wa nyada za nyanda za juukusini.

Akizungumza
baada ya kukamilika kwa kazi hiyo Mhandishi Mazingira kutoka Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji, Daniel Manase alisema mafuriko hayo yaliyoharibu
kingo yenye urefu wa takribani mita 180, yalisababisha kingo za mto
kubomoka n ahivyo mto kuacha njia ya asili nakuanza kupita kwenye mkondo
mpya uliojitokeza.

Aliongeza kwakusema kuwa Kuhama kwa mto
kulipelekea banio la skimu ya Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni kukosa maji na
mazao yaliyokuwa shambani yalikauka, Mhandisi Manase Alisema, baada ya
kufika katika eneo hilo nakuona hali halisi kazi kubwa ilikuwa
nikutengeneza barabara ya muda kwanza ili kuweza kufika katika eneo
liliko haribika kutokana na mazingira kutokuwa rafiki.

Alisema, Kazi ya ujenzi iliendelea kwa kujaza mawe na vifusi katika ujenzi wa tuta ili kulimmarisha.

“Pamoja
na kwamba tulikuwa na vifaa vyetu, tulipata msaada wanyongeza ya
eskaveta, kutoka kwa muwekezaji Kilimanjaro express anayefanya uwekezaji
katika maeneo hayo, nakufanya kazi usiku na mchana karibia masaa 29,
ili kuweza kuzunguka na kuziba gema maana maji yalikuwa yanakula
gema.”Alibainisha.

“Tulizunguka kwa umbali wa kilometa 25 ili
kuweza kubeba mawe na vifusi kuhakikisha kazi inakamilika, mwanzoni
tulikuwa tunazunguka umbali wa kilomita tano kutokana na kwamba hali
haikuwa nzuri ikabidi tuzunguke hizo kilomita 25.”Alisisitiza Mhandisi
Manase.

Mhandisi Manase alisema, Kazi ya kupandisha tuta ilikuwa
na changamoto ya mvua kutokana na kwamba vifaa vilikuwepo, magari
yaliyokuwa yakikwama yalikwamuliwa.

Aliendelea kusema kuwa
kwasasa kazi hiyo imekamilika na wananchi katika maeneo hayo wanaweza
kuendelea na shughuli za kilimo katika skimu ya Ruaha mbuyuni kama
kawaida kwani hali ya mazingira sasa imesharudi katika hali yake ya
kawaida.