Moshi Ndugulile na Mapuli Kitina Misalaba
Umoja wa wanawake wa
CCM Tanzania U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini leo wamefanya kongamano lililojumuisha
takribani wanawake 400,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake
Duniani
Kongamano hilo limefanyika
leo Machi 12,2024 katika ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo limejumuisha
uwakilishi wa wanawake kutoka makundi mbalimbali wakiwemo wastaafu, viongozi wa
taasisi na asasi za kiraia, wajane,
wajasiliamali, wenye ulemavu,na viongozi wa wanawake wa jumuiya zote za chama
cha Mapinduzi CCM ngazi ya tawi, kata hadi Mkoa.
Katika kongamano hilo
zimewasilishwa mada mbalimbali ikiwemo mwanamke na uongozi,ujasiliamali,ukatili
wa kijinsia pamoja na mada inayohusu maadili na ndoa.
Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi, katibu
wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo amesema
mmomonyoko wa maadili unatokana na Ndoa zenye migogoro isiyokwisha hivyo amewataka
Wanawake kusimama imara katika jukumu la kuwajibikia nafasi yao kama Mama na
viongozi katika ngazi ya familia na jamii.
Ametoa wito kwa Wanawake kuwa na umoja na mshikamano
na kupaza sauti za kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto.
Amezungumzia pia uchaguzi wa serikali za mitaa
baadaye Mwaka huu na uchaguzi mkuu utakaofanyika Mwaka kesho 2025 kwamba
Wanawake wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya
Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewaomba Wanawake kuendeleza umoja na
mshikamano ili kusukuma maendeleo mbele.
Nhemanilo amewaomba Wanawake kuendelea kuiunga mkono
serikali katika juhudi na hatua za kufikia mafanikio.
Akizungumza katika kongamano hilo katibu wa Chama
cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) amewataka
Wanawake wa Wilaya ya Shinyanga kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika badaye Mwaka huu 2024 na
uchaguzi mkuu utakaofanyika Mwaka kesho 2025 ili kuleta uwiano baina yao na
wanaume katika nafasi za uongozi.
Amesema ili kwenda sanjari na kauli mbiu ya
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mwaka huu 2024 inayosema wekeza kwa
wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii, Wanawake wanapaswa
kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ili kuweka uwiano sawa wa
Wanaume na Wanawake katika uongozi.
Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Msanii
Richard Masele amesema chama hicho kinatambua mchango mkubwa wa wanawake katika
maendeleo na ustawi wa Nchi.
Naye naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban ameeleza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na serikali kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni msukumo na usimamizi mzuri wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaofanywa na wabunge pamoja na madiwani.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga
Bi. Odilia Batimayo akizungumza katika kongamano hilo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga
Bi. Odilia Batimayo akizungumza katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Rehema
Nhamanilo akizungumza katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Rehema Nhamanilo akizungumza katika kongamano hilo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya
Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) akizungumza kwenye kongamano hilo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya
Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) akizungumza kwenye kongamano hilo.
Katibu wa itikadi, siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Msanii Richard
Masele akizungumza kwenye kongamano hilo.
Wanawake wakiendelea na Burudani kwenye kongamano
hilo.