Vijana wa kanisa la abc tabata jijini dar es salaam watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

 Vijana
wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Tabata Mandela jijini
Dar es Salaam na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mandela wakiwa katika
picha ya pamoja kabla ya kwenda kutoa msaada kwa waathirika 20 wa
mafuriko na wazee wasiojiweza wanaoishi mtaa huo wa jana. Kulia ni 
Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC, Flaston Ndabila.
 Mkutano kabla ya makabidhiano wa msaada huo ukifanyika.
 Vijana wa kanisa hilo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi sh.50,000 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mandela Yusuph Nyombi. 
 Msafara ukielekea kutoa msaada kwa waathiri wa mafuriko.
 Msafara ukielekea kutoa msaada kwa waathiri wa mafuriko.
 Msafara ukielekea kutoa msaada kwa waathiri wa mafuriko.
 Mwenyekiti
wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila
(kushoto), akimkadhi msaada huo, Mariam Rashidi. Kutoka kulia ni Wajumbe
wa mtaa huo, Leonard Chalema na 
Tablisa Bushir.
  Mwenyekiti
wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila
(kushoto), akimkadhi msaada huo, Chande Shomari. Katikati ni Mjumbe wa
mtaa huo, 
Tablisa Bushir.
 Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Lusiana Mkono.
 Mwenyekiti wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila (kushoto), akimkadhi msaada huo, Piamaria John.
 Vijana wa kanisa hilo, wakimkadhi msaada huo, Khadija Mussa kwa niaba ya Mme wake, Juma Mwengele.
 Mwenyekiti
wa Community Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila
(kushoto), akimkadhi msaada huo, Naomi Mlowe ambaye vitu vyake na
chakula vilisombwa na maji.
 Msaada huo ukitolewa kwa familia ya  Hassan Mbega ambayo nyumba yao na  vitu mbalimbali na chakula vilisombwa na maji. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC, Flaston Ndabila.
Msaada huo ukitolewa kwa familia ya  Omari  Issa ambaye ni mgonjwa. 
 
 
 
Na Dotto Mwaibale
 
VIJANA
wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Tabata Mandela jijini
Dar es Salaam wametoa msaada kwa waathirika 20 wa mafuriko na wazee
wasiojiweza wanaoishi Mtaa wa Mandela.
 
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Community
Health Workers (CHW) wa kanisa hilo, Gadi Ndabila alisema wameguswa
kusaidia waathirika hao na sio mara ya kwanza kusaidia jamii katika eneo
hilo.
 

Kila wakati tumekuwa na desturi ya kusaidia jamii inayotuzunguka hapa
kanisani na baada ya kutokea mafuriko na baadhi ya wananchi kubomokewa
na nyumba na kusombwa kwa vitu vyao pamoja na chakula tukaona tuwafariji
kwa kuwanunulia chakula na vitu vingine” alisema Ndabila.
 
Alitaja
baadhi ya vitu walivyotoa kuwa ni unga wa sembe, mafuta ya kula pamoja
na sabuni vyote vikiwa na thamani ya sh.900,000 ambazo zilitokana na
kuchangishana na kupata ufadhili kutoka kwa muumini mmoja wa kanisa hilo
anayeishi Marekani Tamari Mwakakonyole.
 
Mbali
ya msaada huo Ndabila alitoa sh.50,000 kwa Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Mandela Yusuph Nyombi zilizotolewa na kanisa hilo kwa ajili ya
kusaidia shughuli mbalimbali katika ofisi ya mtaa huo.
 
Akipokea
msaada huo Nyombi aliwashukuru vijana hao na Askofu Mkuu wa Makanisa ya
ABC, Flaston Ndabila kwa msaada huo na kuwa kanisa hilo linatakiwa
kuigwa na watu wengine.
 

Kanisa lenu limekuwa likigusa maisha ya watu kiroho na leo sio mara
yenu ya kwanza kutoa msaada kwa jamii nakumbuka umewahi kutoa msaada kwa
yatima, wazee na hata katika ofisi yangu nilipoanza kazi mwaka 2015
mlitusaidia kutununulia vifaa vya ofisini hakika ninyi ni watu wenye
upendo wa hali ya juu” alisema Nyombi.
 

Napenda kukushukuru Baba Askofu na uongozi wote wa kanisa lako kwa moyo
mliouonyesha kwa wahanga hawa wa mafuriko hakika unastahili pongezi
kubwa Mungu akaifungue milango yenye heri kwako na timu nzima ya vijana
walioguswa na kutoa msaada huu,  mmetenda mambo makubwa mno hakika Mungu
akawalinde kwa moyo huu mlionao wa kusaidia watu kila leo naamini
atazidi kuwa bariki na kuwafungulia milango ya riziki  hatuna cha
kuwalipa ila yeye atawalipa” alisema Mjumbe wa Serikali ya mtaa huo,
Tablisa Bushir.
 
Akizungumza
katika makabidhiano ya msaada huo Askofu, Flaston Ndabila alisema ili
kuunga mkono jitihada za Rais Dkt.John Magufuli katika sekta ya elimu
kanisa hilo kwa kusaidiwa na familia ya Fanuel Leonard  itawasaidia
kuwanunulia vifaa vyote vya shuleni wanafunzi 50 kuanzia darasa la
kwanza hadi sekondari ambao hawana uwezo kabla ya kuanza masomo mwezi
Januari mwakani.
 
Alisema kazi inayofanyika hivi sasa ni kuwahakiki wanafunzi hao ili kubaini kama kweli hawana uwezo na wanahitaji msaada.
 
Akitoa
shukurani kwa niaba ya wenzake Mzee Chande Shomari alishukuru kanisa
hilo kwa kuwapa msaada huo ambao umetolewa kwa wakati baada ya
kuathiriwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha mwanzoni mwa wiki
hii na kuharibu miundombinu ya barabara, nyumba na kusomba vitu vya
ndani pamoja na chakula.