Viongozi wa vyama vya ushirika watakiwa kutotumia fedha za wanachama bila idhini ya mkutano mkuu wa chama.

SALVATORY NTANDU

Viongozi
wa Chama cha  Ushirika wa  akiba na mikopo SHIRIKISHO SACCOS LIMITED
wilayani  Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutotumia fedha za
wanachama kinyume na makisio yalioridhiwa  na mkutano mkuu na badala
yake ili kuondoa migogoro isiyokuwa na tija.

Hayo
yamebainishwa na Daniel Kimatha na Prisca Agustino kwenye mkutano mkuu
wa mwaka wa SHIRIKISHO SACOSS LIMITED uliofanyika Mjini kahama ambao
ulikuwa na lengo la kutathimini hoja mbalimbali zinazokikabili chama
hicho kwa mwaka 2019 na kuangalia namana bora ya kuzipatia ufumbuzi.

Wamesema
kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongzo katika shirikisho hilo kutumia
fedha kinyume na makisio yaliyoridhiwa na mkutano mkuu wa mwaka na
kusababisha kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wanachama wao na badala
yake wanapaswa kuwashirikisha kabla ya kufanya matumizi.

“katika
mwaka huu wa 2019 viongozi wetu wametumia shilingi laki mmoja kinyume
na makisio yalioridhiwa na mkutano mkuu suala hili halikubaliki
walipaswa kutushirikisha,alisema Kimatha.

Akijibu
hoja hizo Mwenyekiti wa {SHIRIKISHO SACCOS LIMITED} Tito  Greyson Okuku
amekiri kujitokeza kwa suala hilo na kusema kuwa walitumia fedha za
faida walizopata kutokana na rida walizokusanya  na kuomba radhi
wanachama hao na kuahidi kuwa suala hilo halitajitokeza tena.

Kwa
upande Dronick Kamugisha ni afisa Ushirika wa Halamshauri ya Mji wa
Kahama amesema kutokana na kasoro mbalilimbali zilizojitokwza katika
chama hicho wao kama Halamshauri wamejipanga kutoa elimu ili wananchama
waelewe dhima ya Ushirika na namna bora ya Uendeshaji.

Naye
Mkaguzi wa vyamba vya Ushirika mkoa wa Shinyanga Rodrick Kilemile 
amesema ofisi yake imebaini vyama vingi vya ushirika hawana wataalamu wa
mahesabu hali ambayo imekuwa ikiwapa shida katika uandaaji wa taarifa
za mwaka na kusababisha kuwepo kwa migororo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *