Virusi vya corona: idadi ya wagonjwa tanzania yafika 147 baada ya wagonjwa 53 zaidi kukutwa na virusi hivyo

Kijana aliyevalia barakoaHaki miliki ya picha
Getty Images

Tanzania
imethibitisha visa vipya 53 vya ugonjwa wa corona nchini humo hatua
inayoongeza idadi ya watu walioathirika na ugonjwa huo kufikia watu 147.

Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari , waziri wa Afya Ummi Mwalimu amesema kwamba wagonjwa wote ni raia wa Tanzania.
Idadi
hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa kwa siku moja katika taifa la Afrika
mashariki tangu wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo kugunduliwa katika
eneo hili.
Amesema kwamba miongoni mwa wagonjwa hao 38 wanatoka
katika mkoa wa Dar es salaam, 10 katika Kisiwa cha Zanzibar , mmoja
kutoka Kilimanjaro , 1 kutoka Mwanza , Pwani Mtu 1 na Kagera mtu 1.
”Munaweza
kuona nimetoa takwimu kubwa sana lakini tumeamua tuseme ukweli kwa
sababu Watanzania sasa lazima waelewe kuwa tunakabiliwa na changamoto
kubwa.” alisema waziri huyo.

Ameongezea kwamba Idadi ya watu waliopona ni 11 huku waliofariki wakiwa 5.
Vilevile amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kubwa kujilinda dhidi ya ugonjwa wa Corona.
“Kama kuna mmoja alikuwa na shauku basi ni wakati afahamu Corona inaanza na wewe kujikinga na pia uwakinge wengine”
Aidha
afisa huyo wa serikali amesema kwamba kuna watu wenye dalili za ugonjwa
wa corona ambao wamekuwa wakienda kupata huduma za matibabu katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kutokana na hilo ametoa wito kwa
hospitali hiyo kutopokea wagonjwa kama hao akisema kwamba Muhimbili ni
hospitali kuu ya rufaa inayokabiliana na magonjwa mengine na badala yake
akawataka wagonjwa hao kuripoti katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya
Amana mjini Dar es Salaam.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa
kwa siku moja katika taifa la Afrika mashariki tangu wagonjwa wa kwanza
wa virusi hivyo kugunduliwa katika eneo hili.

Waziri wa Afya nchini Tanzania Ummi MwalimuWatanzania watenga siku tatu za maombi

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Rais John Pombe Magufuli wa
Tanzania kuwaomba raia wa taifa hilo kutenga siku tatu kuanzia tarehe 17
hadi 19 Aprili 2020, kumuomba Mwenyezi Mungu ili kuwaepusha na janga la
ugonjwa wa corona.

Mikutano ya ibada inaruhusiwa nchini Tanzania.
Katika chapisho lake la mtandao wa Twitter Magufuli aliwataka raia wa taifa hilo kusali na kwa imani yake Mungu atawasikia.

Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia.

Wazanzibari waonywa dhidi ya kujitibu

Kulingana
na taarifa hiyo wagonjwa hao ni kati ya umri wa miaka 20 hadi 66 na
hawana historia yoyote ya kusafiri nje ya nchi katika siku za hivi
karibuni.
Waziri huyo wa Afya amewasisitizia wananchi ambao wana
dalili za homa kali, kukohowa na kupiga chafya kujitokeza katika vituo
vya Afya au kupiga simu nambari 190.
” Ni vyema mgonjwa mwenye
dalili za maradhi haya asijichanganye na wagonjwa au watu wengine na
tuache tabia ya kujitibu wenyewe kwani kwa kufanya hivyo tutendelea
kueneza maambukizi na vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo”, alisema
bwana Hamad Rashid katika taarifa yake.