Waandishi wa habari mkoa wa shinyanga waipongeza tcra

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wameipongeza na
kuishukuru mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kwa kuwakumbusha kuendelea
kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta ya mawasiliano ya
kielektronik na posta.

Wametoa pongezi hizo leo Jumatano Juni 21,2023 baada
ya kushiriki kwenye
semina
 iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania TCRA kanda ziwa ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Empire Hotel Mjini
Shinyanga.

Waandishi hao wamesema watahakikisha wanaendelea
kusimamia na kuzingatia sheria za vyombo vya habari katika utekelezaji wa
majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza kwenye semina hiyo Meneja
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis
Mihayo amewakumbusha mambo mbalimbali yanayohusiana na mamlaka hiyo.

Mhandisi Mihayo pamoja na mambo
mengine amewataka waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuzingatia sheria na
taratibu za Nchi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha amewasisitiza kufanya
kazi kwa weledi, kuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na taratibu
za  TCRA katika kutoa huduma stahiki
kwenye jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Bwana
Edwin Soko ambaye amewezesha mada 
inayohusu sheria za uandishi wa habari amewakumbusha waandishi wa habari
Mkoa wa Shinyanga
kuepuka kuandika habari za uchochezi na udhalilishaji huku
akisisitiza
uzingatiwaji wa maadili na miiko iliyowekwa kwa mujibu
wa sheria hizo.