Waandishi wa habari mtandaoni ‘blogs & online tv’ wapigwa msasa kuhusu haki za binadamu

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) vinavyohusisha mitandao ya kijamii zikiwemo Blogs na  Online TV  kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuandika kwa wingi habari za utetezi wa haki za binadamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 20,2019 na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu Jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa  utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi huo unaratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.


Gwandu alisema ni vyema waandishi wa habari wa vyombo vya habari wakatumia mafunzo wanayopewa na kuonesha kwa vitendo namna gani mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa yanawasaidia katika kazi zao.

“Washiriki wa Work Group Three inayohusisha waandishi wa habari mtandaoni tutimize wajibu wetu kwa yaliyo ndani ya uwezo wetu, bado hatujaona habari za haki za binadamu na demokrasia kama ambavyo tunatakiwa kufanya”,alisema.

“Tunaendelea kufuatilia kwa makini namna gani tutapunguza washiriki katika kundi hili, wafadhili wetu wameendelea kujiuliza na kuhoji kuhusu mafunzo tunayopewa na wajibu wetu”,

“Nyinyi ni watu wazima mjitathimini mmesafiri kutoka kwenu kuja kushiriki mafunzo yanayogharamiwa kwa fedha nyingi,halafu hatuoni mabadiliko makubwa,hatutasita kupunguza washiriki ili tubaki na wale wanaozingatia kinachofundishwa”,aliongeza Gwandu.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Froldius Mutungi akizungumzia kuhusu haki alisema, haki za binadamu hazirithiwi wala kutolewa na mtu hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kulinda haki za binadamu na kupaza sauti pale haki zinapovunjwa.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu mjini Dodoma yaliyoshirikisha waandishi wa habari mtandaoni (Blogs/Online Tv ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media). 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Froldius Mutungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Froldius Mutungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Froldius Mutungi  akitoa mada kuhusu haki za binadamu.

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *