Waandishi wa habari watakiwa kuwa mabalozi kubadili mifumo hasi inayokandamiza wanawake kwenye uongozi
Afisa Programu – Sera na Ujenzi wa
Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana akifunga warsha ya Waandishi
wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya
kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake
kwenye nafasi za uongozi. Picha na Kadama Malunde 1 blog

 
Na Shushu Joel – Dar es salaam
Waandishi wa habari wametakiwa kuwa
mabalozi katika kuandika habari za kubadili mitazamo hasi ya jamii juu
ya wanawake kutokuwa viongozi katika jamii.Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba
18,2019 na Afisa Programu – Sera na Ujenzi wa Vuguvugu TGNP
Mtandao,Shakila Mayumana wakati wa akifunga warsha ya Waandishi wa
habari ngazi ya jamii kutoka mikoa ya Shinyanga,Tabora,Simiyu,Mara na
Kigoma yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya
kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za
uongozi.


Mayumana amesema endapo wanahabari
wakitumia kalama zao wataisaidia jamii kuondokana na mila hasi katika
jamii zinazomnyima fursa mwanamke kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa.
“Waandishi wa habari ni watu
wanaokubalika na kuthaminika katika jamii hivyo tunawaombeni mtumie
fursa hii ya elimu mliyoipata hapa ili mkaisaidie jamii zetu ziondokane
na mifumo hasi inayomgandamiza mwanamke”
,amesema.


“Naomba washiriki wa warsha hiii
muende kufanyia kazi yale yote mliyojifunza katika kuhamasisha wanawake
na vijana kushiriki katika uchaguzi. Fanyeni kazi zitakazotengeneza
historia na kumbukumbu katika maeneo na jamii mnayoishi”
,ameongeza Mayumana.


Warsha hiyo ya siku tatu imefanyika
Septemba 16,2019 hadi Septemba 18,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao
Jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa wanawake
na uongozi unaotekelezwa na TGNP Mtandao na UN Women.
Lengo kuu la warsha hiyo ni kuwajengea
uwezo waandishi wa habari juu ya kutoa taarifa zenye mrengo wa kijinsia
hasa zenye kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo
kubadili mitazamo na mila hasi zinazozuia ushiriki wa wanawake katika
uongozi.

 Afisa
Programu – Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana
akifunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga
kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo
kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi. Picha zote na Kadama Malunde 1 blog

Afisa Programu – Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana akiwahamasisha Waandishi
wa habari kuwa mabalozi katika kuandika habari za kubadili mitazamo
hasi ya jamii juu ya wanawake kutokuwa viongozi katika jamii.

Afisa Programu  Mwandamizi TGNP Mtandao,Deogratius Temba akizungumza wakati wa kufunga warsha ya
Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu
namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa
wanawake kwenye nafasi za uongozi. 

Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi
wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo akielezea namna UTPC
inavyozingatia usawa wa kijinsia katika masuala ya uongozi.
Mkufunzi wa Masuala ya Jinsia na Uongozi (Mwezeshaji) Andulile Mwabulambo akizungumza wakati wa kufunga warsha ya
Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu
namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa
wanawake kwenye nafasi za uongozi. 


Afisa Habari TGNP Mtandao,Monica John akizungumza wakati wa kufunga warsha ya
Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu
namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa
wanawake kwenye nafasi za uongozi.