Wadadisi sensa ya kilimo wakutana arusha

AWALI akimkaribisha Mgeni Rasmi Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu 

KATIBU  Tawala wa mkoa wa Arusha akifuangua Mafunzo ya siku tatu ya Wadadisi wa Sensa ya Kilimo Mifugo na Uvuvi iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mapema leo jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mafunzo hayo yaliofunguliwa na Naibu waziri wa kilimo jijini Mwanza mwishoni mwa wiki picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Meza kuu wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi wa Sensa ya kilimo uvuvi na mifugo mapema leo jijini Arusha yaliondaliwa na Ofisi ya ya Taifa ya Takwimu Kutoka Kushoto ni Meneja wa Takwimu mkoa wa Arusha Leokadia Mtey akifuatiwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta Katibu Tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega akifuatiwa na Afisa Mwandamizi Ofisi ya Taifa yaTakwimu Robert t Kasililwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mali Hargeney Chitukuro

Wadadisi wa mafunzo hayo kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Arusha hayupo pichani mapema leo jijini Arusha kama walivyokutwa na kamera ya matukio kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shele ya sekondari Arusha jijini hapa

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega mapema leo jijini Arusha