Wadhibiti wa ubora wa elimu nchini wapewa elimu ya amali

Egidia Vedasto,
APC Media Arusha.

Idadi ya Wathibiti Ubora wa Elimu 340 kutoka chini nzima wameanza mafunzo ya elimu ya amali yatakayowezesha kuboresha kiwango cha elimu ya votendo na kuzalisha wanafunzi watakaoweza kujitegemea kimaisha baada ya kumaliza masomo.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Uthibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mwalimu Ephrahim Simbeye amesema mafunzo hayo yataleta mabadiliko makubwa kutokana na watoa mada wabobezi walioandaliwa kwa ajili ya mafunzo hayo.

Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu ya Sayansi na Teknolojia Mwalimu Ephraim Simbeye (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Ualimu Huruma Mageni (kushoto)

Aidha amewasihi Wathibiti Ubora kuwasikiliza kwa umakini watoa mada ili elimu hiyo iwasaidie na wengine waliobaki ofisini kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu na kuingia katika mashindano ya Kikanda na Kidunia.

“Ndugu zangu nyinyi ndio TBS wa Elimu na jiicho la Wizara, mkishirikiana na kukaa pamoja naamini mabadiliko yatakuwa makubwa, tunategemea mafunzo haya yawe endelevu na yenye kuleta tija, msiwe wachoyo wa kuwaelimisha wengine ili kufikia malengo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kama inavyotakiwa”mesema Simbeye.

Hatahivyo amewataka kuthibiti ubora wa ndani ya shule, kushirikisha jamii katika masuala ya maendeleo ya elimu, kusimamia unasihi na ushauri nasaha kama ilivyo katika suala la maadili.

“Nawakumbusha kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa Mkoa wa Arusha ili kuliingizia Taifa mapato, hii inawezekana kukifanyika utaratibu mzuri ili mkafurahie mandhari na utajiri uliopo katika vivutio hivyo” ameongeza Simbeye.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Ualimu Huruma Mageni amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kutokana na umuhimu wa elimu ya amali iayolenga kuleta chachu na matokeo makubwa katika teknonojia na kujitegemea.

“Pongezi zetu ziwaendee Wawezeshaji na Maofisa Kamisheni kutoka Wizara ya Elimu, NACTEVATE na VETA watakao fundisha mpangilio na mtaala wa amali na fani za amali, utaratibu wa kusajiri shule za amali, muundo wa kuandika tathminiya amali na mengine mengi” amefafanua Mageni.

Pia Mthibiti Ubora Elimu wa Halmashauri ya Wilaya Newala Mkoani Mtwara amesema wawezeshaji wameanza kutoa mwanga na maelekezo kuhakikisha elimu y amali inaboreshwa.

“Kwa upande wangu changamoto ninazoziona ni upungufu wa walimu katika shule za amali, vifaa vya kufundishia na miundombinu michache kwa maana ya maktaba na maabara” ameeleza Rashid.

Mthibiti Ubora kutoka Halmashauri ya Handeni Mkoani Tanga Telesia Kapinga amesema mafunzo hayo yatawapatia elimu ya kujitegemea na kuanzisha viwanda vidogovidogo.

Mafunzo hayo yatafungwa Desemba 02, na yamebeba Kaulimbiu “Utoaji wa Elimu Bora ya Amali hutegemea Tathmini Makini ya Ufundishaji na Ujifunzaji”.