Wafanyabiashara wapewa siku 5 kuondoa mifugo katika mnada wa kizota

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.
Pauline Gekul akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa mifugo katika
mnada wa Kizota wakati alipotembelea mnada huo kukagua shughuli
zinazofanyika ambapo amewapa siku tano kuhakikisha wanaiondoa mifugo yao
wanayoitunza kwenye mnada huo ikisubiri kwenda kuchinjwa. (16.03.2021)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.
Pauline Gekul akizungumza na watendaji wa mnada wa kizota, viongozi wa
halmashauri ya Jiji la Dodoma na viongozi kutoka WMUV wakati
alipotembelea mnada Kizota kukagua shughuli zinazofanyika ambapo
ameagiza ujenzi wa ukuta katika mnada huo uanze haraka. (16.03.2021)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.
Pauline Gekul akikagua miundombinu iliyopo katika Mnada wa Kizota wakati
alipotembelea mnada huo kukagua shughuli zinazofanyika. (16.03.2021)

Wafanyabiashara wa mifugo katika Mnada
wa Kizota Jijini Dodoma wametakiwa kuacha kuhifadhi mifugo yao
inayokwenda machinjioni katika eneo la mnada kwani kufanya hivyo ni
kinyume na taratibu.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul leo (16.03.2021) wakati alipotembelea
mnada huo kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika ambapo pia
alikutana na baadhi ya wafanyabiashara wa mifugo.

Gekul amewaeleza wafanyabiashara hao
kuwa zipo taratibu za uendeshaji wa Minada ya Upili ambapo mifugo
ikishanunuliwa inatakiwa kuchukuliwa na sio kutuzwa hapo ikisubiri
kupelekwa machinjioni.

“Hivyo natoa siku tano kwa
wafanyabiashara wote ambao mnatunza mifugo yenu hapa mkisubiri kuipeleka
machinjioni kuhakikisha mnaitoa na kuitafutia eneo jingine kwa ajili ya
kuitunza,” alisema Naibu Waziri Gekul.

Aidha, Naibu Waziri Gekul aliwaeleza
wafanyabiashara hao kuwa wizara imeshatenga fedha zaidi ya milioni 200
kwa ajili ya kuanza kuboresha miundombinu ya mnada huo ikiwa ni pamoja
na ujenzi wa ukuta unaozunguka mnada huo.

Vilevile ametoa rai kwa wananchi
kutovamia eneo la mnada, kwani moja ya sababu iliyochelewesha kuanza kwa
ujenzi wa ukuta huo ni migogoro iliyotokana na uvamizi wa ardhi. Pia
amewataka viongozi katika ngazi ya Kata, Mitaa na Vijiji kuhakikisha
wanasimamia na kuchukua hatua mapema pale wanapoona mtu anavamia maeneo
haya ya minada.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,
Joseph Mafuru amesema kuwa timu ya wataalam inayofanya uhakiki wa eneo
hilo kutokana na uvamizi itakapomaliza kazi yake watahakikisha
wanalipima eneo hilo kwa haraka